JINA LA KITABU: BARUA KWA DADA

  MUANDISHI : MAHDI IDALATIYANI

KIMECHAPISHWA:NA TAASISI YA UTAMADUNI

CHAPA: YA KUMI NAMOJA

CHAPA: YA KWANZA MWAKA 1382

  MWAKA:1384.

KWA JINA LA MWENYEENZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

BARUAKWA DADA

UFAFANUZI WA MASUALA YANAYOHUSIANA NA UMUHIMU WA KUVAA HIJABU

Salamu alaikum dada mpendwa.

Barua yako ambayo umeniandikia nimeisoma.

Mimi suala la kuvaa hijabu kwa kumuiga mama yangu tu na bila ya kujua umuhimu wake silikubali, kwani sitaki niwe ni miongoni mwa wenye kuabudu mila zisizokua na msingi, sitaki kutolewa thamani, wala kua niko nyuma bali nataka niwe kama walivyo watu wengine katika jamii, mimi sitaki kutekeleza matakwa ya wazee bila ya kujua malengo yake, kwanza hasa nataka muniambie ni wapi Qur’ani imemtaka mwanamke avae hijabu? La pili ni kwa nini wanaume wawe huru na wawe wanatenda walitakalo, lakini wanawake wawe wamewekewa mipaka na vikwazo, na kwa nini hamutaki watu kuwawacha huru na kuyawachia mambo yaelekee kwa mtiririko wake wenyewe, kwani mkifanya hivyo mtaisalimisha jamii kutokana  na msuguano, nyinyi mmeifanya dini kua nzito na mambo mkayafanya magumu, mpaka mmefikia kumtaka mwanamke hata kama atakua yupo peke yake na akataka kusali basi ni lazima avae hijabu, hivi nyinyi mmemfanya Mungu kua ni mwanamme kiasi ya kwamba sisi tujistiri mbele yake? Nataka kujua hasa kutokuvaa kwangu hijabu kunamdhuru nani katika jamii? Mimi najipamba nitakavyo na ninavaa nguo nitakazo, mambo yangu mimi yanakuhusuni nini? Mimi sifanyi hivyo kwa ajili ya kuleta ufisadi, halafu ni kwa nini hamuwaambii wanaume wasiwaangalie wanawake bali mnatuambia sisi tuvae hijabu? Samahani msije mkanifikiria mimi kua sina dini au ni kafiri, amini usiamini mimi ni kama wewe namkubali Mwenyeezi Mungu na vile vile naikubali Qur’ani nami ni muumini wa kweli, na wala sitaki kukosa radhi za Mwenyeenzi Mungu, mimi sio miongoni mwa wale wasiojua fadhila, naelewa kuwa Mwenyeenzi Mungu amenipa neema chungu nzima, mimi niko katika bahari ya neema zake, na napenda kila siku nizidi kuwa karibu nae, na nimridhishe zaidi, na niwe muangalifu zaidi katika masuala tofauti, na niyaelewe undani wake masuala hayo, ili niishi katika njia iliyo sawa, na siyo niishi kama vile wanavyotaka watu, mimi nasema kwamba iwapo kuna watu chungu nzima wasiokuwa na hijabu basi kuvaa hijabu kwangu mimi kutakuwa na faida gani? Itakapokuwa kutokuvaa hijabu kwangu mimi kutasababisha watu kupotea basi tujaalie kwamba mimi nitavaa hijabu lakini kuna watu wangapi wasiovaa hijabu? Ambao bado watakuwa ni kizuizi na watakuwa ni sababu ya kuwapoteza watu, basi kuvaa au kutokuvaa hijabu kwangu mimi kuna tofauti gani? Ukiachia yote hayo lakini hebu nambieni hivi nyinyi ni kwa nini mnayafanya mambo kuwa ni magumu, na hata nywele moja ya mwanamke hamutaki ionekane, mimi nataka kuelewa nywele moja ina tatizo gani kuonekana, na italeta madhara gani, wewe ni lazima unipe mimi haki katika suala hili, na baadae nataka unieleze ni kitu gani kitakachonifanya mimi niwe na hijabu, na vipi mimi nitaweza kulikubali suala hili.

JAWABU

Kwa kweli barua yako nimeipata na imenifikia, na kusema kweli mwanzo nilikuwa sina shauku ya kukuandikia jawabu kuhusu masuala yako, lakini baadhi ya ibara zako zimenilazimisha mimi kukamata kalamu na kukujibu, ingawaje ni kwa ufupi kabisa, na ibara zenyewe zilizonisababisha

Kujibu ni hizi zifuatazo:

Mimi sitaki kufanya jambo nisilolijuwa malengo yake.

Mimi naikubali Kur-ani.

Mimi napenda Mwenyeenzi Mungu awe radhi nami.

Baada ya kuziona ibara hizi nikasema mwenyewe kwa mwenyewe:

Nitamuandikia ukweli ulivyo, itakapokuwa ni kweli anataka kuelewa ukweli ulivyo na iwapo ni kweli wewe unatafuta radhi za Mwenyeenzi Mungu basi utatoa muda wako kwa ajili ya kuyafikiria mambo haya, na utaitupia macho kur-ani, na pale utapoona.

 kwamba maneno yangu yana ushahidi wa Kur-ani na yanakubaliana na akili basi utayakubali, na iwapo wewe utakuwa huko katika kutafuta ridhaa za Mwenyeenzi Mungu na wala hutaki kuujuwa ukweli, na kwa kweli samahani sivyo kama vile mimi nnavyofikiria hivi kwa nini usiwe ni mwenye kutafuta radhi za Mwenyeezi Mungu, na ni kwa nini usitake kuujuwa ukweli? Kwani hii dunia na vilivyomo ndani yake vina thamani gani? Vitakavyomsababisha mtu aridhike na maisha haya mafupi ya dunia, na kutupilia mbali mambo ya kiakili na ya imani, na kuyafumbia macho mambo hayo, mimi nnaelewa kwamba wewe unataka kufahamu, na unataka kuishi katika jamii kwa kupitia ufahamu wako na kuelewa kwako,na kwa sababu mimi nimefahamu hilo ndio maana nikaamuwa kuijibu barua yako. Ili jawabu yako iwe wazi zaidi nimeamuwa maneno yako kuyafupisha katika vipengele kumi, na nnakuandikia kwa ajili yako, kisha naanza kujibu kipengele kimoja kimoja, nafanya hivyo kwa kutegemea kuwa maelezo yangu utayasoma kwa uangalifu, na utakaa katikati bila ya kutilia uzito upande Fulani, na nakutaka uyaangalie kwa makini, na lile utakaloliona ni sawa basi likubali:

1.    Kutokuwa na hijabu kwa wanawake kuna madhara gani kwa watu wengine.

2.    Hivi katika Qur-ani suala la ulazima wa kuvaa hijabu kwa wanawake limezungumzwa

3.    Kuna msukumo gani unaoweza kulifanya suala la hijabu kuwa ni la lazima na kwa lugha nyengine, nini hasa falsafa ya kuvaa hijabu?

4. Kwa nini hamuwaambii wanaume wasiwaangalie wanawake, ili wanawake waepukane na shari ya kujifunika maguo.

5.    Ni kwa nini wanaume wamepewa ruhusa ya kufanya walitakalo na wavae watakavyo, lakini wanawake wakawekewa vazi maalum

6.Ni sawa kabisa mimi silitilii maana suala la kuvaa hijabu, na nnavaa nguo nzuri na kujipamba kisha nnatoka mbele za watu, lakini sina makusudio ya kusambaza upotofu na ufisadi.

7.Kwa kupatikana watu wengi wasiokuwa na hijabu kwa hali yoyote ile ufisadi utapatikana, basi kuvaa au kutokuvaa kwangu mimi hijabu kutakuwa na tofauti gani?

8.Itakapokuwa wanawake wote wana uhuru wao basi suala hili litakuwa ni la kawaida katika jamii.

9.Kwa nini hata nywele moja ya mwanamke haitakiwi kuonekana, huu unywele mmoja wa mwanamke una madhara gani kuonekana.

  10. Hivi ni kwa nini mwanamke atakapokuwa peke yake ndani ya nyumba na akawa anasali ndani                                      

 Anatakiwa kuvaa hijabu?

 JAWABU:

1. Kutokuvaa hijabu wanawake kuna madhara gani kwa wengine?

Katika kujibu suala hili kwanza naanza kukusimulia maneno ya mwana biashara mmoja, yeye anasema hivi uislamu unataka aina ya ladha za kijinsia uzitenge kwenye masuala ya ndoa tu, ladha hizo ziwe za aina yoyote ile, za kuangalia kwa macho au za kugusana kimwili, na masuala ya ndani ya jamii yawe yana uhusiano na mambo ya kikazi za kijamii, tofauti na mfumo au mtizamo uliokuwa sio wa kiislamu ambao kazi za kijamii na masuala ya kijinsia yanaendana pamoja, kwa hiyo uislamu unataka kutofautisha masuala mawili haya.

Kwa maoni yako ikiwa sehemu za kufanyia kazi, sehemu za kutafuta elimu, kufanya tahakiki, kuzalisha au kukuza vitego  tofauti vya kiuchumi ikiwa zitakuwa zimeepukana na wasiwasi wa masuala ya kishetani na mambo ya uchafu maendeleo yatakuwa ni mengi na bora zaidi au ikiwa sehemu hizo zimezungukwa na masuala machafu ya kijinsia yanaweza yakapatikana maendeleo bora?

Kutokuwa na hijabu kwa wanawake na kuwepo mchanganyiko baina ya wanawake na wanaume katika sehemu za kazi ndiko kunakosababisha madhara na uharibikaji wa jamii, ambapo ikiwa watu watayazingatia masuala haya basi kutaipelekea jamii kuishi kwa amani bila ya ufisadi na wala hakuna mtu yoyote sio mwanamke wala mwanamme ambae hatoridhika na hali hiyo.

Dada mpendwa mimi nna uhakika kwamba ikiwa utazingatia haya nnayokuandikia, na ukafahamu kwamba kuna madhara gani yanaweza kutokea kwa watu na jamii kwa ujmla ikiwa masuala ya kutokuvaa hijabu hayatatekelezwa, na wewe mwenyewe hutokuwa tayari kushuhudia madhara hayo.

Mimi nakuandikia kwa ufupi tu madhara ambayo yanaweza kutokea katika jamii ikiwa masuala ya kuvaa hijabu hayatozingatiwa.

KUTOKUWEPO NA USALAMA KIAKILI

 

Itakapokuwa wanawake na wanaume wanachanganyika pamoja itapelekea matamanio ya nafsi kwa watu na jamii, na kama inavyoeleweka kwamba nafsi ya mwanaadamu haitosheki,na kila siku zinapokwenda inazidi kuongozeka kama moto ambao unachocholewa kwa kuni, na mwanaadamu akishafikia katika hali hii ni tabu sana kujirekebisha, katika hali hii basi utamkuta mwanaadamu amepoteza mahitajio yake, matokeo yake anakuwa ni mwenye tabia mbaya za kishetani, asie jiamini, na mwenye wasi wasi.

KUPUNGUKIWA NA MAPENZI NA FAMILIA YAKE

Mwanamme ambae kila siku atakuwa anaonana na wanawake ambao wamejipamba na wasiovaa hijabu, na akawa anakabiliana nao katika pirika zake za kikazi za kila siku, akawa anaona uzungumzaji wao, tabasamu zao, na wakati anaporudi nyumbani akamkuta mke wake katika hali isiyokuwa nadhifu, amechoka na kazi za nyumbani za mchana kutwa hatokuwa na shauku hata hata ya kumuangalia mke wake, katika hali hii basi mwanamme huyo atakuwa na nguvu za kumlinganisha mke wake na wanawake ambao amewaona nje, matokeo yake atadhania kwamba haiwezekani kuishi na mke wake na mwisho wa mambo utakuta anamuacha mke wake, na mara nyingi utakuwa umeshashuhudia au umeshasikia kwamba mwanamme fulani ameoana na mfanyakazi mwenziwe, na mke wake wa mwanzo amempa talaka.

Kuongezeka kiwango kikubwa cha talaka ni kuongezeka kwa watoto wakimbizi, na watanga na njia wasiokuwa na kazi, na kama utazingatia mara nyingi watoto kama hao ni tofauti iliyotokea baina ya wazazi wao, na kutokupendana na kutosikilizana baina ya mke na mume katika kuendeleza maisha yao.

Dada mpendwa kwa maoni yako wewe unafikiri ni kwa nini vijana wa zama hizi hawapendi kufunga ndoa? Katika zama za zamani wanawake walikuwa ni wenye heshima na wenye kuhifadhika zaidi kuliko zama za sasa hivi, kila kijana alikuwa akipendelea kufunga ndoa, na walikuwa wakiowa wakiwa na miaka kidogo tu (yaani baada ya kubaleghe), ama bahati mbaya katika zama zetu hizi za sasa hivi tunaona kwamba vijana wengi wanapopendelea kukidhi mahitajio yao ya kibinafsi huenda kutafuta watoto wa watu, au hutafuta wanawake ambao masuala ya hijabu kwao wao sio muhimu, na wanapofunga ndoa ni kwa sababu tu wamelazimishwa na wazee wao, na wanakuwa hawana furaha katika maisha yao.

Hivi ni kweli kama ingelikuwa vijana hawawaoni wanawake katika hali ya kujipamba na kutembea bila ya hijabu hali ingelikuwa ni hii hii? La ! sifikirii,

Ni mtu gani anaekubali kuona familia yake, au watoto wake wako katika hali hii ya maisha?

Hivi mwanamke ambaye haoni umuhimu wa kuvaa hijabu, na anajipamba na kutembea barabarani, au sehemu za kazi hivyo anaelewa kwamba anakiuka sheria za Mwenyeenzi Mungu? Au inawezekana anafanya hivyo kwa kukusudia.

KUDHAIFIKA KAZI ZA KIUCHUMI NA KIUTAMADUNI KATIKA JAMII

Dada mpendwa mimi nakuuliza suala:

Katika sehemu za kazi ambazo ni wanawake watupu au wanaume watupu, kazi zinakuwa zinafanywa kwa mazingatio zaidi au katika sehemu ambazo kila siku na kila wakati wanaume wanakabiliana na wanawake katika hali ya mapambo na kutokuwa na hijabu?

 Hivi katika skuli au katika vitengo vya kujipatia elimu ikiwa wanafunzi wanawake na wanaume wako pamoja na wana maelewano katika masuala tofauti ikiwa ya kijinsia au hata namna ya kuvaa kwao kwa nguo, kutembea kwao, mazungumzo yao n,k…….katika hali hii wana nafasi ya kushughulikia masomo yao, au ikiwa skuli za wanafunzi wa kike na wakiume mbalimbali?

 Ni jambo lililowazi kwamba mchanganyiko wa wanawake na wanaume, na kutozingatia masuala ya kujistiri au kuvaa hijabu ndiyo inayosababisha kuharibika kwa mioyo au akili za baadhi ya wanawake na wanaume, na kupelekea kutokufanya kazi vizuri, mbali ya haya inatokea wakati unamkuta kijana anapenda kufanya kazi na kukuza uchumi, lakini anapokumbana na ufisadi katika jamii yaani anapokuwa na uhusiano na wanawake ambao hawajistiri au hawavai hijabu utamkuta mtu huyo hana shauku ya kufanya tena kazi na anakuwa wakati wote yuko katika fikra potofu za kujenga uhusiano na wanawake hao, matokeo yake kijana huyo anaishia jela au anakuwa ni mvuta bangi, basi kutokea kwa matatizo haya ingelikuwa kijana huyo alisema na nafsi yake na akawa hayuko tayari kujishughulisha na ufisadi huo angelikutwa na matatizo hayo?

4.KUTOKUWEPO NA USALAMA NA KUONGEZEKA HIYANA.

Wezi siku zote wanaendelea kuiba na kufosi mali za wengine, ama mtu atakapokuwa yeye mwenyewe hatafanya hadhari na akauwacha wazi mlango wa gari yake au mlango wa nyumba yake, au dhahabu na fedha zake, akawa hakuzihifadhi, basi mtu huyo atakuwa yeye mwenyewe amewatangazia wezi ghanima, kwa sababu kufanya kwake hivyo kunawarahisishia wezi kazi. Basi mambo ndio hivyo hivyo kwa upande wa watu wenye maradhi ya moyo, na wenye kuabudu matamanio yao, wanapomuona mwanamke aliekuwa hajajihifadhi au amejipamba hali akiwa ndani ya jamii ya watu mambo hayo yanawachochea zaidi na kuwasindikiza katika ufisadi, hapo basi huanza kumfuata fuata mwanamke huyo na kumuudhi, na inaweza kupelekea mwanamke huyo kuvunjiwa heshima yake au hata kupoteza roho yake, kuna wanawake wangapi hadi leo walioingia katika mikono ya mafisadi na kupata matatizo mbali mbali, iwapo wewe utakuwa umehudhuria mahakamani au umeyakagua mafaili ya vikundi vya kihuni yaliyoko mahakamani, utakutia kwamba waliotiwa mikononi  na vikundi hivyo miongoni mwa wanawake wamepata mateso kutoka katika vikundi hivyo na hadi kupoteza roho zao,na wanawake hao waliopata matatizo hayo walikuwa ndani ya jamii hawajihifadhi kwa kuvaa nguo za heshima, na kwa bahati mbaya matokeo kama haya ya hatari yamezidi kuwa mengi katika jamii, na nna uhakika kabisa kwamba wanawake hao waliopata matatizo walikuwa hawana malengo ya kuvuruga amani katika jamii, na wala walikuwa hawajachoshwa na maisha ya duniani, lakini wao walikuwa wakipendelea tu kuonekana katika jamii huku wakiwa wanatembea barabarani, na hali wakiwa wamevaa nguo wazipendazo, huku wakiwa wao wameghafilika na matokeo yatakayotokea baadae, basi kudumu kwa vitendo kama hivyo kunasababisha kutopatikana amani ya mtu binafsi na katika jamii.

5.KUPUNGUKA KWA THAMANI NA HESHIMA YA MWANAMKE NDANI YA FAMILIA PAMOJA NA JAMII

Iwapo wanawake hawatojitangaza katika jamii na hawatayaonesha mapambo yao, na badala yake Wakayafanya hayo mbele ya waume zao basi kila mwanamme ataijuwa thamani ya mke wake na atampa heshima maalum, na neema ya uzuri itakuwa ni nyenzo na changamoto ya maisha katika kuhifadhi heshima ya kifamilia, ama iwapo utafikia wakati kwamba mwanamme kwa urahisi kabisa atakuwa ni mwenye kuwaona wanawake chungunzima barabarani na kuwatupia macho pamoja na kuwa na uhusiano nao, basi hapo nafasi asili ya mwanamke, na sifa maalum alizokuwa nazo zitakuwa ni zenye kusahaulika na badala yake mwanamke atakua ni kama chombo cha kujistareheshea au kuchezewa na wanaume tofauti, na katika taratibu kama hizi mwanamme atakuwa hamthamini mkewe, na atasahau ladha ya chumvi, kwa sababu kiwango chochote kile cha wanawake akitakacho atakipata kwa sababu wako wengi wamemwagwa barabarani, ni maana mbaya ilioje iliyobeba sentensi hii, na ni makosa mazito yalioje kwa wale wenye kusababisha thamani ya mwanamke ishuke hadi kufikia kiwango hichi, na chenye kuumiza zaidi ni kule kupata nafasi watu wenye kuabudu pesa na wenye kuabudu dunia katika kuwaharibu wanawake na kuwafanya wao ni bidhaa, bali bidhaa ina thamani zaidi.

Ni jambo la kusikitisha mno kuona kwamba kwa ajili ya kutafuta soko la magazeti, na kwa ajili ya kutafuta pesa, utakuta juu ya gazeti huchapishwa picha ya mwanamke, au kwa ajili ya kuwavuta wateja utakuta mtu anamuweka mwanamke dukani, na kwa ajili ya kuwavutia watizamaji watu hutafuta film za wanawake wenye kujionesha, jee! Kufanya hivyo si moja kati ya njia za kumvunjia mwanamke heshima, na kuitoa thamani nafasi ya mwanamke? Na jee wanawake ambao hawajihifadhi na macho ya wengine hivi hawasababishi kuvunjiwa heshima wao wenyewe pamoja na wanawake wengine?

Suala la wanawake kuwafanya ni chombo na kutumia vibaya uzuri wa nyuso zao limeenea kiasi ya kwamba baadhi ya wakati utakuta katika gazeti kuna nyuso za wanawake ambao ukiwaangalia utaelewa kwamba wana ujuzi Fulani, na wanatoa ujumbe fulani, na wenyewe wanaamini ubaya huo, wanakiri suala hilo, basi angalia maneno haya ya mchezaji wa snema maarufu anavyokiri:

“mimi mwenyewe ni nyota nikimaanisha kwamba sio mtu ambae nnadhamini na kuzifanya film zinunuliwe, watowaji makosa na wasambazaji magazeti katika masuala ya film zangu wao hawaangalii sana namna ya uchezaji wangu wa snema, bali wanaangalia kitu chengine, katika zama hizi mimi nnajihisi vibaya sana, na kitu kibaya kabisa ni kwamba mchezaji wa film hufikia wakati yeye mwenyewe akajua  kwamba watizamaji wanakuja kuangalia sinema kwa ajili ya uso wake wenye kupendeza, na wala sio kwa ajili ya namna ya uchezaji wake wa film, mimi mwenyewe nimeufikia uhakika huu mchungu, na nimeamua kufikiria upya kabisa kuhusu na uchezaji wangu wa film.

 Ni sawa matokeo haya ni mabaya yalioje kwamba badala ya mtu kuangalia sanaa na uzuri wake au kutupia jicho elimu pamoja na kuangalia juhudi, juhudi ambazo zinampelekea mtu kuongeza ujuzi wake, basi jamii hutupia macho na kuangalia nyuso na matamanio yao.

 Ama ni lazima tupate jawabu la suala hili lisemalo ni mtu gani ikiwa wanawake watazingatia masuala ya kuvaa hijabu na kujistiri, na wasikubali kuwa ni kama chombo cha kustareheshea kinachotumiwa na wanaume, basi ufisadi huu ambao sasa umeenea katika jamii utatoweka.

  Sasa hivi nnaifafanua  nukta ya pili ambayo uliielezea.

MASUALA YA KUVAA HIJABU KWA WANAWAKE YAMEELEZEWA KATIKA QUR_ANI?

Ndio masuala ya kua ni lazima kwa wanawake kuvaa hijabu yameelezewa wazi katika Qur-ani, Kuna sehemu mbili katika Qur-ani ambazo zimeelezewa ulazima wa kuvaa hijabu kwa wanawake.

Moja ni katika Suratul Nuur aya ya 30 na 31, na sehemu nyengine ni katika Suratul-Ahzaab aya ya 59.

Lakini kutokana na umuhimu wa kuvaa hijabu kuna sehemu nyengine mbali mbali katika Qur-ani ambazo zimeelezea kuhusu umuhimu wa kuvaa hijabu, lakini katika sura hizo mbili ambazo nimezitaja hapo juu yamezungumzwa kwa uwazi kabisa, mimi nitakuandikia kwa ufupi mandhuri ya aya ya 30 na 31 ya suratu nnur, lakini na wewe mwenyewe pia nenda kaangalie katika tafsiri .

Katika aya hizi kumeelezewa nukta hii:

A.  Wanaume wametakiwa kutowaangalia wanawake, kwa kusudi la matamanio yao.

B.    Wanawake wametakiwa kutowaangalia wanaume, kwa kusudi la matamanio yao.

C. Wanawake wamekatazwa kutoonesha mapambo yao.

D.  Kuvaa hijabu na kujistiri kuanzia kichwani, shingoni, kifuani, kwa kuvaa hijabu au shungi ambalo linaweza kuustiri mwili wa mwanamke.

E.    Kuna baadhi ya viungo vya mwanamke ambavyo sio lazima kujistiri mfano, uso na viganja vya mikono.

F.     Wanawake wamekatazwa kujijalibisha mbele ya wanaume ambao ni haramu kwao.

Katika nukta zote hizo ambazo nimeziainisha sehemu iliyokuwa muhimu zaidi na yenye kuhusiana na mada yetu ni nukta ya c na d, ambazo nukta hizi tutazielezea kwa undani kabisa.

KUKATAZWA KWA WANAWAKE KUTODHIHIRISHA MAPAMBO YAO.

Aya inasema

Na wala wanawake wasiyadhihirishe mapambo yao ila yale mapambo ambayo haiwezekani kuyaficha,(mfano wa viganja na uso).

Neno pambo katika maana ya kilugha lina maana hii:

Ni kwamba kitu ambacho kinaweza kumvutia mwanamme

Katika maneno ya kilugha za kizamani tunasoma:-

Nzuri ni kinyume cha mbaya, na pambo ni kile kitu ambacho kinaweza kumvutia mtu kwa uzuri wake, basi kwa hakika pambo yaani ni kile kitu kizuri kinachoweza kumvutia mtu, kitu hicho kinaweza kuwa ni asili au sio asili, kwa hiyo pambo la mwanamke ni kila kitu ambacho kinamfanya  mweanamke apendeze na awavutie watu.

Kwa hiyo tunaweza tukaligawa neno pambo katika sehemu mbili .

PAMBO: 1. Pambo asili: mfano nywele za kichwani.

2.    Pambo lisilo la asili: nalo ni miongoni mwa rangi, nguo, au bangili na herini,rangi ni mfano wa vitu ambavyo wanatumia wanawake kwa ajili ya kujipamba sura, nguo mfano wa hijabu za rangi zilizonakshiwa na zenye kujalibisha.

Sasa kwa vile neno pambo tayari limefahamika basi hatuna budi kurejea tena aya ya Qur-ani ambayo tuliifafanua mwanzo. Yaani wanawake wasiyadhihishe mapambo yao ila yale ambayo haiwezekani kuyaficha.

Ukizingatia maana ya neno pambo na mifano niliyoiainisha, utaelewa kwamba katika aya hii tukufu Mwenyeenzi Mungu hawaruhusu wanawake kudhihirisha mapambo yao kwa wanaume ambao ni haramu kwao kuwaonyesha mapambo hayo, mfano Nywele za kichwa, kujipamba uso, kuvaa nguo ambazo zinaweza kuwavutia wanaume, pete, herini, bangili nk..

Na aya inaendelea kama hivi ifuatavyo “ila kwa yale mapambo ambayo hayawezekani kuyaficha”

Ukizingatia na tafsiri za hadithi zilizotafsiriwa na Maulamaa wa kidini, mapambo ambayo siyo lazima kuyaficha ni uso nao ni mpaka sehemu ambazo tunaosha kwa ajili ya kutia udhu, na viganja vya mikono mpaka mwisho wa vidole,  haya ni mapambo ya asili, ama mapambo ambayo sio ya asili au pete ya uchumba ambayo inaonyesha kwamba mtu huyo tayari ameshafunga ndoa  na ikawa pete hiyo haitowajalibisha wanaume basi pia sio lazima kuificha, mbali ya mapambo hayo mapambo mengine ni lazima kuyaficha.

Ama nukta nyengine inayofuata ni kwamba:

Kuistiri shingo, kifua kwa kuvaa shungi, hijabu, au hata mtandio, aya inaendelea hivi:

“Wal-ya-dhribna bikhumurihinna ala juyubihinna” yaani

“Na wajifunike mashungi yao mpaka vifuani mwao”

 Neno “khumri” wingi wake ni “khimaar”  lakini katika maana yake ya asili ni hijabu.

Ama katika lugha rahisi ni nguo ambayo hutumia wanawake kwa ajili ya kujistiri vichwa vyao, (yaani ni kilemba au shungi)

Neno juyuub wingi wake ni jiyb, likiwa na maana ya kitambaa ambacho hutumia wanawake kwa kujistiria, kabla ya kuteremshwa aya hii wanawake walikuwa wakivaa hijabu hawajistiri mpaka vifuani mwao, yaani walikuwa wakiwacha shingo na vifua vyao wazi, na ndipo Allah (s.w) alipoiteremsha aya hii kuwaamrisha wanawake ya kwamba wanapovaa hijabu wajistiri shingo zao na vufua vyao.

Basi kwa maelezo hayo  na aya ambayo tumeifafanua utakuwa umeshafahamu kwamba masuala ya kuvaa hijabu yameelezwa katika Qur-ani, na Mwenyeenzi Mungu amewaamrisha wanawake kuitekeleza amri hiyo, ama maelezo yanayofuata ni kwamba kuna hekima gani na malengo gani katika kuvaa hijabu?

HEKIMA NA MALENGO YA KUVAA HIJABU

Dada mpendwa wewe uliuliza kwamba una malengo gani mpaka uvae hijabu, na usivae nguo za zinazokwenda na wakati na kujipamba?

JAWABU: Mimi nna uhakika kwamba kama utakaa na kufikiri kwa makini kuhusu suala hilo basi ni lazima utafahamu malengo ya kuvaa hijabu.

Kwa maoni yangu mimi mwanamke yoyote atakaesoma maelezo hayo ataelewa umuhimu na malengo ya kuvaa hijabu.

KUDHIHIRISHA URAFIKI KATIKA KUMPENDA MOLA

Hakuna shaka wewe ushashuhudia baadhi ya watu walio karibu nawe, inawezekana rafiki, au mtu mwengine yoyote mkawa mmekinaiana na akatumia lugha mbali mbali za kukuonesha wewe kwamba anakujali na ni rafiki wake wa karibu sana, ikatokea siku ukawa na shida na ukamfata mmoja wa rafiki zako hao na kumuomba akusaidie kiasi fulani cha pesa, lakini akakujibu kwamba yeye pia anahitaji kusaidiwa pesa na wewe, siku nyengine ukamwambia akuazime kitabu akakujibu kwamba yeye vile vile anataka kusoma, fikiria kila unapokuwa na shida anakuzungusha huku na huku kuonesha kwamba hataki kukusaidia, wewe unaweza kumfikiria nini mtu kama huyo,

Bila ya shaka utasema ni rafiki gani huyu anaenipoza kwa maneno tu?

Sasa fikiria uhusiano ulionao wewe na Mola wako, sisi binaadamu kila siku tunajionesha kwamba ni wapenzi wa Mola wetu, ama mambo tunayoyafanya hayamridhishi.

Basi malengo bora kwako wewe kuhusu masuala ya kuvaa hijabu ni kumtaka mola wako ambae anakupa rizki na kila mahitaji ambayo unayataka, nayeye ni rafiki bora zaidi miongoni mwa rafiki zako, basi kwa nini usikubali na kuyatekeleza yale ambayo ameyaamrisha na anayaridhia? Ili kuonesha kwamba na wewe umeridhika kuwa na urafiki nay eye?

KUMSHUKURU MWENYEENZI MUNGU KWA NEEMA AMBAZO AMEKUJAALIA

Binaadamu wakati anapokwenda kuwaangalia wagonjwa hospitali atashuhudia vijana wengi wamelala vitandani, na pengine hawawezi kuinuka mpaka kwa kusaidiwa, hawana neema ya uzima, wanaomba Mungu awaondoshee maradhi hayo ili waweze kuinuka kwa miguu yao, hapo mwanaadamu anaweza kufahamu kwamba Mola wake amempa neema ya uzima lakini yeye hazingatii wala hafikirii, uzima na uzuri ni moja ya neema kubwa ambazo Mwenyeenzi Mungu amewakirimu waja wake, basi binaadamu hatuna budi kushukuru neema hizo, basi tuwe tayari kufuata yale ambayo ameyaridhia Allah (s.w) na tusimuasi Mola wetu.

Dada mpendwa wakati unapojiangalia katika kioo zingatia kwa makini neema ambazo amekujaalia Mola wako, angalia macho yako kama ungelikuwa huna macho ungelikuwa na tofauti kiasi gani na wenye macho, basi hivi kweli inaelekea kutokana na neema ambazo ametujaalia Mola wetu tumuasi yeye na tumfuate shaitani?.

Dada mpendwa nakuomba uyaangalie maelezo haya kwa makini, itokee siku unatembea na mwanao njiani  ukiwa na matunda mkononi na uwakute watoto wanacheza, uwagaie matunda hayo watoto hao, na baadae wasikushukuru, wale matunda hayo na yatakayobakia wampige nayo mtoto wako wewe utawafanya nini au utasema nini juu ya watoto hao?

Mwenyeenzi Mungu hana mtoto, lakini binaadamu ni waja wake, basi akitokea mwanamke ambae Mola amempa neema ya uzuri na uzima, na kwa kutumia neema hizo akamkufuru Mola wake kwa kufanya yale asioyaamrisha Mola mwanamke huyo atakuwa na tofauti gani na watoto hao?

Ndio, kushukuru neema ambazo ametujaalia Mola mfano wa uzuri na uzima, ni sababu muhimu ambayo itakufanya uwelewe lengo na umuhimu wa kuvaa hijabu.

KUMPOKONYA SILAHA SHETANI

Adui mkubwa wa mwanaadamu ni shetani, naye ameapa kwamba ni lazima ampotoshe binaadamu. Na ndio maana utaona sehemu zenye kitega uchumi na pesa nyingi watu wengi hughilibiwa na shetani, kwa sababu sehemu kama hizo shetani ndipo anapopata nafasi ya kuharibu amani ya mwanaadamu, sasa ikawa sisi ndio sababu inayomfanya afanikiwe na tusiyakubali yale ambayo Mola ametuamrisha na tukamfata shetani.

Hakuna shaka kwamba kutokuvaa hijabu kwa wanawake na kujipamba ndio sababu kubwa inayomfanya mwanamme aghilibiwe na shetani, kuna wanume wangapi ambao walikuwa ni wacha Mungu lakini baada ya shetani kuwaghilibu kwa kupitia wanawake wamekuwa ni wenye kumuasi Mola wao, na baada ya kuwa walikuwa ni watu wa peponi , wamejipalilia moto wenyewe na wamekuwa ni watu wa motoni.

 Mtume wetu Muhammad (s.a.w) anasema “Kuwaangalia wanawake kwa matamanio ni sawa na mshale wa sumu unaotoka kwa bilisi.

 Yaani ikiwa muwindaji hatoweza kuwinda paa, na kwa kutumia mshale akampiga paa huyo mguuni na kumfanya asiweze kutembea, baadae akaharakia kwenda kumchukua paa huyo.

 Basi kwa kuzingatia mfano huo shetani nae anapotaka kumghilibu mwanamke au mwanamme kwanza humtia wasi wasi mpaka amuone tayari keshamughilibu, ndipo humdhoofisha amani yake na kidogo kidogo humvuatia upande wake.

 Basi kutokana na maelezo hayo tumeelewa kwamba moja katika madhumuni ya kuvaa hijabu ni kwamba kila mwanamke muislamu awe na itikadi ya kupigana na shetani ili asiweze kumughilibu, na asikubali kutumiwa na shetani ili kumkufuru Mola wake.

KUWEPO KWA USALAMA WA WATU NA JAMII

Mwanamke ambaye havai hijabu, na mwenye kujipamba ndio chanzo cha kuwafanya wanaume wenye maradhi kumfata, na tatizo hili ndilo linasababisha jamii isiwe na usalama, kama ambavyo nilielezea mwanzo kwamba vijana wengi wa kiume walio wahuni ndio wanowaharibu wanawake wasiokuwa na hijabu. Basi kwa ajili ya kuhifadhi usalama wa watu na jamii hakuna budi kuelewa kwamba ikiwa wanawake watakuwa na malengo ya kuvaa hijabu jamii itakuwa iko katika hali ya usalama.

KUTOKUSAIDIA WENGINE KATIKA KUFANYA MAKOSA AU KUTO KUSHIRIKIANA NA WATU WENGINE KATIKA UPUUZAJI SHERIA.

Baadhi ya wanawake ambao hawavai hijabu na ni wenye kujipamba wakati wanapotembea njiani husema kwamba, “sisi sio kwamba tunawafanyia hiyana waume zetu, na wala sio kwamba tunataka kuleta ufisadi katika jamii, na wala hatuko tayari kuona watu wanaleta ufisadi katika jamii, na wala hatuko tayari kuona wanaume wanatufuata ili kututumia kama ni vyombo vya starehe, kwa wanawake kama hawa basi ni vizuri kuwambia kwamba nyinyi mnalinda heshima yenu na utu wenu mbele ya wanaume lakini ni lazima wazingatie maelezo haya yafuatayo:

 Kabla ya kuanza kuzungumzia kuhusu maelezo hayo ni lazima tufahamu kwamba suala la kuvaa hijabu ni suala ambalo ameliamrisha Mola wetu, na sisi hatuna budi kumtii yeye, ikiwa suala hilo linapelekea uharibikaji wa jamii, au hata ikiwa haipelekei uharibikaji wa jamii, baadhi ya wakati unaweza kumuona kijana mwanamme anamfuata mwanamke ambae hakujistiri au hakuvaa hijabu lakini kwa vile mwanamke huyo anaweza kumtukana mwanamme kutokana na kumvunjia heshima, mwanamme huyo tayari anakuwa keshatiwa wasiwasi na shetani na baada ya kuwa kamkosa mwanmke huyo huenda kutafuta mtoto wa watu wa kike na kumharibia maisha yake, matokeo yake utakuta mtoto huyo wa kike anatengana na familia yake, na inakuwa ndio sababu ya mtoto huyo kuhitilafiana na wazazi wake, sababu ya yote haya chanzo chake ni Yule mwanamke wa mwanzo aliesababisha matatizo hayo. Hakuna budi kukuelezea kisa kimoja ambacho kimetokea, na nna hakika kwamba huwezi ukasahau hata siku moja, baada ya kuwa kijana mmoja mwaname tuliekuwa tukizungumza kuhusa hali ya maisha ya kila siku, kijana hayo alinambia kwamba kila ufisadi na kufuru unayoijuwa wewe chanzo chake kinatokana na mimi, maneno hayo alimtamkia baada ya kumuelezea matatizo yaliyomkuta mimi sikuelezea kwa sababu sio vizuri kumtangazia mtu aibu yake.

Dada mpendwa kama wewe utafikiria kwa makini utaelewa kwamba kama ingelikuwa sio Yule mwanamke ambaye hakuwa na hijabu basi madhambi yote haya yasingelimfika Yule kijana mwanamme aliemuona mwanamke huyo na akatiwa wasi wasi na shetani kumfata mwanamke huyo, lakini yeye hana habari na haya, na baadae anasema mimi sina kazi na mtu na wala sina nia ya kufanya ufisadi katika jamii, na siko tayari kuona mwanamme ananivunjia heshima yangu wakati yeye ameshiriki katika madhambi yote hayo na yeye ndio chanzo cha matatizo yote.

ATHARI NYENGINE

Mbali ya hayo niliyokuelezea kuvaa hijabu kwa mwanamke wa kiislamu kunawasababishia wengine kutokana na mwanamke huyo kuwa karibu na Mola wake, wavutiwe na tabia za mwanamke huyo na wao wafanya yale ambayo Mola wao anataka, hivyo tunaweza kuwagawa watu katika makundi matatu.

1.    Watu wema na wanadumu katika uongofu wao.

2.    Watu aliokuwa sio wema ambao wanakubali makosa waliofanya na wanapojirekebisha huwa thabiti katika msimamo wao, watu walio katika makundi haya mawili ni kidogo sana.

3.    Watu wa kundi la tatu wanategemea hali ya jamii ilivyo, ikiwa jamii iko katika tamaduni nzuri na wao hufuata namna ya utamaduni wao ulivyo, na ikiwa jamii haiko katika tamaduni nzuri na wao vile vile hufuata  namna ya utamaduni wao ulivyo.

Kwa hiyo watu ndio wanayoifanya jamii iwe nzuri, na vile vile ndio wanayoifanya jamii iwe mbaya. Mtume (s.a.w) anasema:-

“ Mtu yoyote ataevumbua jambo jema, kisha akalizowesha kwa watu kiasi ya kwamba baada yake yeye kukawa na watu wengine wenye kuliendeleza jambo hilo,basi mtu huyo hulipwa thawabu kwa kila wanapolitenda watendaji wa jambo hilo, bila ya kupunguziwa kitu watendaji hao katika thawabu zao, mtu yoyote atakaeanzisha au kuvumbua jambo baya, kisha akazowesha watu kulitenda au akalieneza kiasi ya kwamba baada ya kuondoka kwake kukawa na watu wanaliendeleza jambo hilo basi mtu huyo atalipwa uovu kwa kila wanapotenda watu hao jambo hilo, bila ya kupunguziwa watu hao kitu chochote katika uovu wao (dhambi zao).

Kuhusiana na utafiti wetu sisi ni lazima tukubali kwamba wenye kuzingatia suala la hijabu na kulitekeleza kisha wakalipigia debe kwa wengine jambo hilo lenye kupendwa na Mwenyeenzi Mungu bila ya shaka watapata bahashishi maalum kutoka kwa Mola wao. Acha niongezee kwa kusema kwamba kufanya hivyo ni ujasiri mkubwa katika upande wa mtu kupigana na nafsi yake.

Unaelewa kwamba moja kati ya vigao vya nafsi inavyogawika navyo ni nafsi ya mwanaadamu ni (Nafsi ammarah) yaani nafsi yenye kuamrisha maovu, nafsi hii siku zote hua inamuamrisha mtu kufanya maovu, baadhi ya Maulamaa wanasema hivi “ mtu mwenye kuitii nafsi yake na kuzipa kichogo amri za Mwenyeenzi Mungu ni mfano wa mtu aliemuokota mtoto wa mbwa wa mwitu mwituni, akamuokota, na kutokana kwamba mtoto wa mbwa wa mwitu alikuwa mdogo, na akawa anamlisha kila aina ya chakula kizuri, huku akighafilika kwamba anamlea adui alie hatari, hali ya kwamba mbwa yule aliekuwa akimlea mtu wa kwanza atakayemla baada ya kuwa mkubwa ni mlezi wake aliyemlea, ingawaje mwanamke ndani ya nafsi yake ana matamanio ya kutokuvaa hijabu na kujionesha kwa watu, ama kwa ajili ya kutaka radhi za Mola wake, basi mwanamke huyo utamuona anajilazimisha kuvaa hijabu, hatua kwa hatua nafsi yake hupata nguvu ya kutenda mema mpaka hufikia kutumia akili na kuangalia vipi Mola anasema katika mambo yote, mtu wa aina hii kwa rahisi zaidi huweza kuimiliki nafsi yake na matamanio ya nafsi, kama vile kupenda ukubwa, kufanya husuda na mengineyo.

KWA NINI HAMUWAAMBII WANAUME WASIWAANGALIE WANAWAKE? KWANI JAMBO HILO LITAWAFANYA WANAWAKE WASIVAE HIJABU

Naelewa kwamba kwa kutokana na hatua nilizozielezea hadi kufikia hapa utakuwa huna haja ya kuuliza suala kama hili, kwa sababu wewe mwenyewe umeshaona kwamba sio kwamba wanaume tuwameambiwa wasiwaangalie wanawake tu, bali kuna msisitizo mkubwa zaidi ya huo, kwani wao ndio wa mwanzo kukatazwa kabla ya wanawake kuamrishwa kuvaa hijabu, kama ilivyo katika Suratun-Nuur, pale Mola alipowataka wanawake kuvaa hijabu, kwanza aliwaanza wanaume kuwaambia wasiwaangalie wanawake, na amemwambia Mtume (s.a.w) akisema “waambie waumini wa kiume wainamishe macho yao.

Ama ni jambo lililowazi kwamba haitoshi kuwaambia tu wanaume wasiwaangalie wanawake mpaka kupatikane matayarisho yatakayowafanya wanaume wasiwaangalie wanawake (yaani kuvaa hijabu), kama ilivyokuwa kuihifadhi mali ya jamii haitoshelezi kuwaambia watu tu kwamba wasiikodolee macho mali ya wengine, na wasiitumie mali ya wengine, bali inahitajika vile vile kuusia watu wasiziweke ovyo ovyo mali zao na wazihifadhi mali hizo, basi ndiyo hivyo hivyo katika sheria za Mola zenye kuihifadhi jamii, pande zote mbili zimeamrishwa kutekeleza wajibu wake, wanaume wasiwaangalie wanawake kwa matamanio, na wanawake nao wasijitangaze kwa wanaume kwa kujipamba na kujiweka uchi.

KWA NINI WANAUME WANA RUHUSA YA KUFANYA WALITAKALO NA KUVAA NGUO WAZIKATAZO? NA WANAWAKE WANALAZIMISHWA KUJIHIFADHI.

Katika kujibu suala hili kunalazimika kusema kwamba, sio kwamba wanaume hawawajibikiwi au hawana wadhifa wowote na dini inawaruhusu kuvaa nguo wazitakazo, lakini kwa sababu lengo la amri zote hizi ni kuhifadhi heshima ya jamii na kuleta amani ya kimwili na ya kiroho katika jamii, na kuzuia shetani na fikra zakezisipenye katika safu za watu, ikiwa mwanamme ataelewa kwamba kuhudhuria kwake katika jamii katika hali maalum, kama vile kuvaa nguo ya mikono mifupi au kujipamba, kutawafanya wengine waingie katika makosa basi atajiepusha kufanya hivyo.

 Ama sababu ya kwamba wanaume sheria haiwabani zaidi katika sheria za kivazi ni kwamba Mola uzuri na kuvutia amekuweka katika kiwiliwili cha mwanamke na wanaume kwa ujumla hawavutii, kiasi ya kwamba wao walazimike kujifunika,basi sheria ya kivazi inaendana na suala la kuvutia na uzuri, ushahidi kuhusiana na maelezo haya ni huu, sisi tumeona katika tarehe aghalabu wanawake ndio wenye kuindwa, na wanaume ndio wawindaji, na mashairi pamoja na visa vya waandishi mara nyingi vinazungumzia uzuri na mvutio wa wanawake, lakini hakujatokea hata mara moja mwanashairi kumsifu mwanamme kwa uzuri wa mwili wake, basi wewe mwenyewe umeona kwamba suala la kutofautisha mwanamme na mwanamke na ubaguzi halipo,bali Mola kwa kutokana na ukweli ulivyo na mambo ya kimwili ya mwanamke na mwanamme pamoja na mambo ya kiroho, ndiyo ambayo yamemfanya Mola azipange sheria kama uzionavyo.

  Ama katika barua yako umeandika hivi:-

MIMI SINA MALENGO YA KULETA UFISADI WALA UPOTOSHAJI

Katika barua yako umeniandikia hivi:

“Ingawaje mimi navaa nguo zinazokwenda na wakati mbele za wanaume, na nnajipamba lakini katu sina lengo la kuleta ufisadi au upotoshaji.

 Kabla ya mimi kutowa msimamo wangu kutokana na maelezo yako na jawabu zako kwanza nna masuala machache naomba kukuuliza, itokee siku umerudi kazini hali ya kuwa umechoka sana kwa kazi, na una haja ya kupata mapumziko, ama jirani yako akawa amefunguwa tivii au redio kwa sauti kubwa, na hana nia ya kukera amefanya hivyo kwa sababu tu anapenda, hivi ni kweli kwa kufanya hivyo hakutokusababishia wewe kutokupumzika?

 Jee! Hivi wewe imewahi kukutokezea siku katika msimu wa baridi ukapanda texi, lakini karibu yako kukawa kuna mtu nanataka kuwasha sigara, kwanza akaomba radhi na kusema kwamba hana budi kuvuta sigara kwa sababu anhisi baridi, hivi ni kweli moshi wa sigara hautokudhuru eti kwa kuwa kwanza ameomba radhi? Na wala hutokasirika?

Jee! Ikiwa mtu amenunuwa bakora mpya kasha akaijaribishia katika kichwa cha mtu ili aijuwe umadhubuti wake, jee kufanya kwake hivyo hakutamletea madhara mtu huyo aliyempiga? Kwa sababu tu yeye hakuwa na makusudio ya kumdhuru, alikuwa na makusudio ya kuijaribu bakora yake tu kama ni nzima.

Basi hivi sasa  baada ya utangulizi huo uliopita tunaweza kupata natija ya kwamba kitu chenye kuleta madhara huwa kinaleta madhara tu, hata kama mtendaji wa kitu hicho hakusudii kuwadhuru wengine, hapo sasa ndio tumefika jawabu ya lile suala lako lisemalo “mimi najipamba na vile vile sivai hijabu lakini sina makusudio ya kharibu jamii, vipi kwangu mimi nitalazimishwa kuvaa hijabu”

WENGI WALIOJE WASIOKUWA NA HIJABU KWANGU MIMI IMEKUWA AJABU?

Kwa kutokana na kwamba kuna watu wengi wasiovaa hijabu, taka usitake lazima jamii itaathirika nao hata kama mimi nitaamua kuvaa hijabu, kwa hiyo kuvaa kwangu au kuto kuvaa kwangu hijabu haina maana yeyote, au hakuleti athari yeyote katika jamii.

 Mimi nna itikadi ya kwamba hata kama wanawakle wote majiani hawatakuwa wakivaa hijabu basi wewe dalili ya kuvaa hijabu, kwani Mola ndie aliyekuamrisha kufanya hivyo.

KWANZA KABISA NI KWAMBA WEWE USIWE NDIYO MUHUSIKA AU MTUHUMIWA KATIKA MAKOSA YANAYOTENDEKA KATIKA JAMII.

 Kila mtu atakaefanya makosa basi yeye ndie mtuhumiwa katika makosa hayo, na ni lazima awe ni mwenye kuhojiwa mbele ya mahakama ya Mola wake.

 Iwapo mtu atakuwa ana habari kwamba usiku wa leyo wezi wana makusudio ya kuivunja nyumba ya jirani yake ambae amesafiri, na akawa na yakini kwamba bila ya shaka mazulio ya jirani yake yataibiwa, kisha katika moyo wake akasema kwa hali yoyote ile mazulia ya jirani yake yatamtoka tu kutoka katika mikono mwake,

 Basi mimi mwenyewe ntayachukuwa haya mazulia, na kabla ya kuja wezi nyumba ya jirani yeye akaenda akayachukuwa mazulia na kuyapeleka kwake, huku akisema nikiyawacha wezi watakuja kuyachukuwa, na nisipoyawacha nitafaidika mimi, kwa hiyo hakuna faida kuyawacha wewe mtu kama huyo utamuhukumu vipi katika tendo hilo alilolifanya? Ikiwa utasema iwapo wakiyachuwa au wasiyachukuwe kwa jirani ni sawa tu, kwani wengelikuja wakayachukuwa wezi kwa hiyo hakuna tofauti ya kuibiwa na jirani au kuibiwa na wezi, cha umuhimu ni kwamba usiku ule mazulia yataibiwa tu, awe ni jirani au mwizi, alipokwenda kuyachukuwa yeye mazulia hakuzidisha kitu katika uovu, ama hapa suala haliko hivyo, kwani hivi sasa baada ya kuyachukuwa yeye ndie atakayekuwa na jukumu, na ndiye atakayetakiwa kulipa hasara, na wangeliyachukuwa wezi basi wao ndiyo wangelikuwa na jukumu hilo.

 Katika upande wa hijabu ndiyo hivyo hivyo, kuwepo wanawake wengi wasiyovaa hijabu kwenye kuwapoteza watu katika jamii, na wewe ukawa miongoni mwao basi nawe vile vile utahusika katika upotoshaji wa jamii.

AMA DALILI YA PILI NI KUHIFADHI HESHIMA NA THAMANI.

 Ikiwa katika jamii uongo utakithiri, na watu wasema kweli wakasema “watu wote hao wenye kusema uongo, usemaji kweli wetu sisi una faida gani?” kisha na wao vile vile wakajiunga na kundi la wasema uongo, na kwa kutokana na kuzidi kwa hiyana katika jamii watu wenye amana nao wakajiunga na kundi la wenye hiyana, na kwa kutokana na watu wengi wasiochunga suala la mavazi, wenye kulithamini suala hilo vile vile wakajiunga na wasiolithamini suala hilo, kama mambo yatakuwa hivyo basi katika jamii mambo yote yenye thamani yatapotea, na kizazi kitakachokuja baadae masuala yenye thamani kubwa katika jamii ambayo tumeyataja hapo nyuma kama vile(amana, ukweli, huruma) yatakuwa ni mageni kwao, na wala hawatoyatambuwa maana yake.

Basi moja kati ya malengo ya kutenda mambo yaliyo sawa hata kama watu watakuwa hawayatilii maanani masuala hayo, ni kuyathamini na kuihifadhi thamani ya mambo hayo, na ikiwa kuna mtu atakuwa anayatekeleza mambo hayo na akawa asirudi nyuma, basi kuna matarajio baadae, mbali ya kule kuihifadhi thamani ya mambo hayo basi atawafanya wengine vile vile, hatua baada ya hatua kujiunga nae, na baadae sifa na tabia njema zitaenea katika jamii.

 Sasa tumefikia kwenye dalili ya tatu ambayo kwa mtizamo wangu ndiyo dalili yenye nguvu zaidi kuliko nyengine:

KUMTII MOLA NA KUZIHESHIMU SHERIA ZAKE.

Bila ya shaka unaelewa kwamba hukumu na sheria za Mola hata kama kuna watu watakuwa wanazipuuza hukumu na sheria hizo, basi sheria hizo zitabakia pale pale na wala hazitofutika, basi hata kama kuna wengi wasiolithamini suala la hijabu, ambalo ni moja kati ya sheria za Mola, basi bado mpango wa Qur-ani kwa nguvu za Mola utabakia palepale na ni lazima uheshimiwe.

 Nukta nyengine ambayo wewe umeiashiria ni hii ifuatayo:

 Hivi iwapo wanawake wote wakiwa huru wewe huoni kwamba mambo yote yatakwenda sawa kabisa?

 Dada yangu, kutoka kwa wengi mimi nimesikia kwamba, katika jamii yetu iwapo watu watakuwa huru katika kufanya makosa na kutokuwa na mipaka maalum ya kisheria, basi mambo yote yatakwenda kikawaida kabisa, na watu hawatokimbilia na kuwa na hamu ya kufanya makosa, mimi vile vile nawafiki suala la (jamii kuwa na hali ya kawaida) ama kwa mtizamo wangu mimi kuna njia mbili ya mambo kuwa ya kawaida katika jamii:

 Njia ya kwanza ni kwamba ufisadi na utendaji wa makosa uwe ni kawaida kwa watu, na uwe ni jambo la kawaida, na ikifikia hivyo jamii itatafuta daraja ya juu zaidi ya ufisadi, na sio kwamba wataacha ufisadi.

Kijana ambaye sigara kwake ni kitu cha kawaida kabisa, inawezekana kijana huyo sigara kwake ikawa ni kitu cha kawaida kabisa ama ikifikia hivyo basi atapanda daraja ya pili na kuelekea kwenye madawa ya kulevya.
Hali ndio hiyo hiyo katika jamii yetu, lilipokuwa suala la kuziwacha wazi baadhi ya nywele za kichwa limeshazoeleka na hakuna mtu mwenye kulistaajabia, basi kuacha wazi ukosi, kufupisha sketi, kupandisha mikono ya nguo, yote hayo yameanza kupamba moto katika jamii baada ya kuzoeleka hilo la mwanzo, basi kuzoeleka na makosa kuwa ni kitu cha kawaida katika jamii, haisababishi watu kuachana na makosa bali inasababisha kuzidi makosa na kufikia katika hali ya hatari zaidi.

 Njia ya pili, ni kuzoeleka kwa natija ya mambo na makosa  katika jamii, kwa mfano, (mwizi akawa ameshazoea kufungwa na kwake ikawa ni kitu cha kawaida), fikiria kwamba kuna mwanamke aliyekwenda kuonana na rafiki yake, na kwa kustaajabu kabisa akamwambia rafiki yake, “kwa nini kibiriti na mashine ya kusagia nyama, umevificha na umeviweka mbali na macho ya watoto?

 Katika nyumba yetu sisi vitu tumeviweka nje nje, na vitu hivyo watoto wanaviona ni vya kawaida kabisa kwa sababu wameshavizowea, kwani mara ngapi wameviona vitu hivyo na vimeshakuwa ni vya kawaida kwao, ama baada ya dakika chache akaulizwa na rafiki yake, kwa nini watoto wako wadogo hujawaleta nyumbani? Akajibu jana tu mmoja kati ya watoto wangu kidole chake alikitia katika mashine ya kusagia nyama na nikampeleka Hospitali, sasa mtu kama huyu ambae vifaa vya hatari amevifanya viwe ni vya kawaida mbele ya watoto basi muwache aonje mashaka na natija ya kufanya kwake hivyo.

 Dada yangu, ukweli uliopo ni kwamba katika jamii za nchi za Europ jambo ambalo sisi tuna shaka nalo ni kutembea uchi, na kutaka uhuru wa kuwa na mafungamano kati ya mwanamme na mwanamke, ambayo yote hayo hakuna shaka ndio yanayosababisha jamii na watu kuharibikiwa, basi ni vizuri kama utafunguwa magazeti ili kuona nini wameandika kuhusu masuala haya ambayo yameleta athari mbaya katika jamii.

 Mimi nitakuandikia habari mbili tatu zinazohusiana na masuala haya, ambazo zimeandikwa katika magazeti, na wewe utaitafuta habari hii na uisome kwa ukamilifu.

 Kutokana na habari za uchunguzi zilizotolewa na Idara inayuhusika na mambo  ya jamii ya London, katika miezi mitatu ya mwaka uliopita, zaidi ya asilimia 31 ya watoto ambao wanaishi London hawana baba.

 Na katika habari za charnel ya Tv ya c.n.n wameeleza kwamba asilimia 50 za watoto ambao wanaishi America watoto wengi wamezaliwa nje ya ndowa, na masuala ya talaka pia ni mengi zaidi.

 Tv ya c.n.n imeonesha film fupi zenye kuonyesha watoto wa kike na wanawake wakitaka msaada kutoka kwa watu na polisi, na wameelezea kwamba makosa ya jinai katika jamii ya Kimarekani yamefikia upeo wake, kiasi ya kwamba idadi za vifo, kuwabaka wanawake, wizi, na aina nyengine za makosa, zinaongezeka siku hadi siku katika miji ya Kimarekani, na polisi hawawezi kuzuia matokeo hayo, kwa hiyo wanawausia wasichana na wanawake kwa ujumla wachukuwe silaha au dawa za kupotezea fahamu ili waweze kukabiliana na mashambulizi na kujihami kutokana na wakorofi

Mimi kwa ukamilifu kabisa nataka kukujibu barua yako ulipouliza:

Ni kwa nini hata unywele mmoja wa mwanamke hautakiwi kuonekana?

Ili liweze kufahamika suala hili kwanza kuna vipengele viwili ni lazima vifahamike:

1.    Sheria zote za Mwenyezi Mungu ambazo zimewekwa  kwa hekima na kwa kutaka kheri na maslahi ya wanaadamu, uchache wake na wingi wake ni lazima zifuatwe, angalia mfano huu (damu ni najisi, ndoo moja ya damu ni najisi, gilasi moja ya damu ni najisi, na hata kiwango cha ncha ya sindano cha damu ni najisi).

Kuiba mali ya watu ni haramu, na hakuna tofauti katika wizi, yaani ukiiba kitu kidogo au kikubwa, vyote hivyo ni haramu.

Suala la hijabu au kivazi ndio hivyo hivyo, kwamba kuonesha nywele mbele ya wanaume ni haramu, sasa iwe ni unywele mmoja au kichwa kizima.

2.    Katika utendaji wa makosa ndio hivyo hivyo kwanza Shetani humdanganya mtu kutenda makosa madogo madogo kisha humpeleka kwenye makosa mkubwa makubwa, dada yangu we! Mimi ninakuuliza hivi ni kwa nini unapomuona mwanao mdogo amechukua pakti ya sigara unamkataza? Hivi ni kwa nini unamkataza? Kwani pakti moja ya sigara ina madhara gani? Nikukuuliza hivyo utaniambia hivi: “a suala si kua yeye amekamata pakti ya sigara, bali ni kua ukimuachia leo akamate kesho ataanza kuvuta sigara moja,na baadaye mbili hadi kuendelea.

Kwa ufahamu, kama ukitaka kukabiliana na tabia mbaya ni lazima uanze kukabiliana nazo tokea zinapoanza kujichomoza, la si hivyo baadae itakua ni vigumu kuzing’oa tabia hizo, ni methali nzuri ilioje isemayo (mwizi wa yai leo ni mwizi wa ngamia kesho).

Hivi sasa ninalijibu suala lako la mwisho lililobakisha alama ya suala ndani ya akili yako:

HIJABU NA MWANAMKE ANAPOKUA NYUMBANI KWAKE

Uliniandikia kua “ hivi ni kwa nini mwanamke akitaka kusali ni lazima avae hijabu hata kama atakua yupo peke yake ndani ya nyumba”?

Dada yangu daima usisahau ya kua Mola wako siku zote huwatakia waja wake kheri na maslahi, na hakuna hata sheria moja ya Mola wako isiyokua na hekima, ima waja waifahamu hekima hiyo au wasiifahamu, hii ni sheria ya Mwenyezi Mungu, vile vile ndani ya sheria hii mna hekima, na miongoni hekima hizo ni hizi zifuatazo:-

1.    Mazowezi ya kumpandisha mtu daraja.

Sala ina fadhila nyingi, na vile vile ni moja kati ya mazowezi ya kumpandisha mtu daraja, ndani ya sala sisi tuna mambo chungu nzima tunayojizoweza nayo, kama vile kumpwekesha Mola, kumkhofu, pamoja na kusoma Qur’ani, basi sala kitu kimoja kilichokusanya mambo tofauti yenye thamani, na hijabu kwa wanawake ndio hivyo hivyo, kama vile Mola asemavyo na Qur-ani inavyosema, hijabu kwa mwanamke huwa inampa thamani maalum mwanamke, na ni moja kati ya mambo yenayomkamilisha mwanamke huyo.

2. Kutangaza rasmi kumtii na kumcha Mwenyeezi Mungu

 Mkuu wa jeshi anawaambia wafuasi wake, “mwanajeshi mzuri na mwenye kujua wadhifa ni lazima siku zote afike uwanjani hali ya kuwa amevaa fomu.

Sasa fikiria iwapo mwanajeshi mmoja atataka kuonana na mkuu wa jeshi wakati anapokwenda Idarani kwake, ikisha yeye avae fomu anapokwenda kuonana nae, kufanya kwake hivyo kutakuwa kutamaanisha kwamba yeye amekubali kufuata amri ya mkubwa wake.

Kwa hiyo basi, kuhudhuria pahali alipokuwepo mkubwa wako huku ukiwa katika utaratibu kamili alioutaka yeye, kutakuwa kunaelezea utiifu wa mtu huyo hata kama hakuzungumza kwa ulimi wake.

Mwanamke muislamu ambaye ameahidiana na Mola wake iwapo atakwenda mbele ya Mola wake na hijabu, kwa ajili ya kutekeleza amri ya Mola wake basi atakuwa yeye anamtangazia Mola kuwa yeye yuko tayari kufuata amri zake na ameridhika na Mola wake.

WASIA WA MWISHO

Dada yangu we mimi nakutaka uyatie akilini na uyafikirie yale yote niliyokuandikia, na jaribu kufikiria zaidi kwamba dunia ni yenye kupita, ujana nao unakimbia kwa nguvu, kuna wangapi waliokuwa wana ndoto za uzuri na walikuwa wakishindana katika kuolewa na leo wako chini ya udongo, na nyuso zao zilizokuwa nzuri pamoja na miili yao haikubakia isipokuwa mifupa tu, kilichobakia ni amali zao tu, iwapo walitenda amali.

Kila mtu katika shule hii ya dunia ana faili lake, na akimaliza shule faili lake bado litabakia, dunia ni soko wako wenye kufaidika katika soko hilo na wako wenye kula hasara, siku zote katika soko hili hutoka watu na kuingia wafanya biashara wengine, basi kama vile unapokuwa muangalifu unapochagua kitambaa unapokuwa dukani, basi amali na matendo yako kuwa muangalifu nayo, na mwishowe niliyokuandikia katika barua hii yachunguze na uyalinganishe, na Mola wako atakuongoza katika njia iliyo sawa.