(KITABU MAFUNZO YA ELIMU YA QUR_ANI)

Saa za kazi

SABABU ZA KUTEREMSHWA QUR_ANI

Hapana shaka inafahamika na kueleweka ya kwamba Qur-ani imeteremshwa kidogo kidogo kutokana na matokeo masuala au mambo tofauti katika kipindi chote, tangu alipopata utume Nabii Muhammad (s.a.w). Aya nyingi za Qur-ani zimeteremshwa kutokana na matokeo tofauti yaliyokuwa yakitokea katika zama hizo, au ziliteremshwa kutokana na masuala ambayo watu walikuwa wakimuuliza Nabii Muhammad (s.a.w), sababu na sharti hizo zinajulikana kwa jina la ( ÇÓÈÇÈ äÒæá) yaani (Sababu za uteremshwaji wa aya za Qur-ani) au (ÔÇÆä äÒæá)  yaani (Misingi ya uteremshwaji kwa aya za Qur-ani).

Ni jambo lililowazi na lisiloshaka ndani yake ya kwamba aya za Qur-ani zilizoteremshwa kutokana na kila sababu au mambo tofauti zinalingana na uteremshwaji wake, kwa hiyo pindi itakapokuwa katika aya kuna neno lisilofahamika maana yake au lenye kutatiza kutamkwa kwake, watu wanaweza kulitatua tatizo hilo na kufahamu kwa undani maana ya neno hilo kwa kurejea namna ya uteremshwaji, wakati, sharti au zama iliyoteremshwa aya hiyo, vile vile kutokana na tokeo lililopelekea kuteremshwa kwake, kwa hiyo ili kufahamu maana kamili ya kila aya ni lazima tufahamu na kuelewa sababu za uteremshwaji wa aya za Qur-ani.

Na tutizame mfano wa aya hii ya (Suratul-Al-Baqarah aya ya 158). Allah (s.w) anasema:-

Åöäøó ÇáÕøóÝóÇ æóÇáúãóÑúæóÉó ãöä ÔóÚóÂÆöÑö Çááåö Ýóãóäú ÍóÌøó ÇáúÈóíúÊó Çóæö ÇÚúÊóãóÑó ÝóáÇó ÌõäóÇÍó Úóáóíúåö Çóä íóØøóæøóÝó ÈöåöãóÇ æóãóä ÊóØóæøóÚó ÎóíúÑÇð ÝóÅöäøó Çááøåó ÔóÇßöÑñ Úóáöíãñ

Maana ya aya hiyo ni kama ifuatavyo:-

“Hakika Safaa na Marwa (Majabali mawili yanayofanyiwa ibada ya kusai huko Makka) ni katika alama au nembo za kuadhimisha dini ya Mwenyeezi Mungu. Basi anayehiji kwenye nyumba hiyo au kufanya Umra, sio kosa kwake kuvizunguka (vilima) hivyo viwili, na anayefanya wema (atalipwa) kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukurani na mjuzi (wa kila jambo)”.

Kuna baadhi ya watu wametowa nadhari zao na kulitilia shaka suala hili ya kwamba, Kusai (alama au nembo) baina ya Majabali hayo mawili ya Safaa na Marwa ni katika nguzo za Hijja na Umra, basi ni kwa nini katika Qur-ani limetumika nenoáÇÌäÇÍ  ? wakati ambapo neno hilo lina maana ya kufanya dhambi?

Na kama tukitizama maana iliyo dhahiri ya aya hiyo itafahamika kwamba Kusai baina ya majabali hayo mawili sio dhambi, basi ibara hii inamaanisha kuruhusiwa Kusai katika Majabali mawili na wala haimaanishi uwajibikaji wa kusai katika Majabali hayo, katika hali ambayo inaeleweka wazi ya kwamba Kusai ni katika mambo yaliyo ya ulazima na ya wajibu katika Hijja, ama kama tukirejea katika sababu za kuteremshwa aya hiyo tutafahamu na kuelewa kwa uwazi kabisa ya kwamba ibara hiyo ni kwa ajili ya kuwaondolea watu shaka kuwa kutokufanya jambo hilo sio dhambi. Ama ni vizuri kama tutafafanuwa kwa undani kabisa kuhusu suala hilo.

Baada ya kufanyika suluhu ya Hudaybia baina ya Waislamu na Washirikina mnamo mwaka wa sita hijria, iliamuliwa na kuafikiwa kuwa Nabii Muhammad (s.a.w) pamoja na Masahaba wake mwaka unaofuata wataenda Makka kwa ajili ya kufanya Hijja ya Umra, katika suluhu hiyo ilielezewa na kukubaliana baina ya Washirikina na Waislamu ya kwamba, Washirikina ni lazima waondoe masanamu yao katika Kaaba na vile vile katika majabali mawili ya Safaa na Marwa kwa muda wa siku tatu ili Waislamu wafanye ibada zao za Kutufu na Kusai wakiwa huru katika sehemu hizo, kwa hiyo baada ya kumalizika muda wa siku tatu Washirikina waliyarejesha masanamu yao hayo hali ya kuwa baadhi ya Waislamu kutokana na dalili au sababu tofauti hawakuweza kwenda kufanya ibada zao muda wa siku tatu hizo walizokubaliana, na ndipo Waislamu walipoingiwa na shaka ya kuwa Kusai baina ya Safaa na Marwa hali ya kuwa kuna masanamu katika sehemu hizo ni dhambi, kwa  sababu hiyo basi Allah (s.w) aliimteremshia Mtume Muhammad (s.a.w) aya hiyo ili awajuulishe Waislamu kuwa wasijizuilie na Kusai kwa sababu Kusai ni katika alama au nembo za Mwenyeezi Mungu. Na kuwepo kwa masanamu ni jambo lisilo asili na lisilotiliwa maanani, kwa hiyo kuwepo masanamu hakutoleta  madhara yoyote yatakayofanya Waislamu wasifanye ibada zao katika sehemu hizo. (rejea kitabu Tafsiri Ayashi, juzuu ya 1, ukurasa wa 70).

Kutokana na maelezo hayo basi, tumeshuhudia kuwa tunaweza kufahamu kwa uwazi maana ya aya hiyo iwapo tutarejea sababu za uteremshwaji wake, ama kwa ibara nyengine, vile vile itafahamika kuwa aya hii haielezei masuala ya uruhusiwaji au uwajibikaji wa Kusai, bali inataka kuwaondolea Waislamu shaka kuwa hakuna kizuizi chochote kitachofanya wajizuilie kutokufanya ibada zao kwa kuwepo masanamu katika Majabali hayo mawili. (Safaa na Marwa).

SABABU NA MISINGI YA KUTEREMSHWA KWA AYA ZA QUR-ANI

Kuna tofauti gani baina ya ibara mbili hizi?

(yaani sababu za kuteremshwa Qur-ani, au misingi ya kuteremshwa Qur-ani).

Wafasiri wengi wa Qur-ani hawakutowa nadhari yoyote kuhusiana na ibara hizo, na matokeo yote au mambo yote yaliyopelekea kuteremshwa aya za Qur-ani wanasema ni ÓÈÈ äÒæá)) yaani (sababu za kuteremshwa aya za Qur-ani) au (ÔÆä äÒæá ) yaani (misingi ya ya kuteremshwa aya za Qur-ani), hali ya kuwa ibara mbili hizi zina maana tofauti, ibara ya pili yaani (misingi ya kuteremshwa aya za Qur-ani) ina maana pana zaidi kuliko ibara ya kwanza (sababu za kuteremshwa aya za Qur-ani), wakati wowote itakapokuwa kuna aya inaelezea kuhusu mtu, jambo fulani, wakati uliopita, wakati wa sasa hivi, wakati ujao, au faradhi za ahkamu, sababu zote hizo zinajulikana kama ni (misingi ya uteremshwaji wa aya za Qur-ani), kwa mfano:-

Kuna aya fulani imeteremshwa na inaelezea kutokana na kutakasika Mitume, au kutakasika Malaika.

Ama sababu za kuteremshwa Qur-ani inatokana na mlolongo wenye kufuatana, (yaani baada ya kutokea matokeo Mwenyeezi Mungu huiteremsha aya), kwa ibara nyengine matokeo yanayotokea ndiyo yanayofanya aya iteremshwe.

MAANA YA KIDHAHIRI NA MAANA YA KIUNDANI YA AYA ZA QUR-ANI (KUFASIRI KINYUME NA MAANA DHAHIRI ILIVYO)

Kutokana na istilaha za kielimu za Maulamaa waliopita wamelifasiri neno ÊäÒíá)) kuwa lina maana ya kuteremshwa au uteremshwaji, kwa maana hiyo basi inawezekana ikawa ni tokeo makhasusi (maalum) au jambo makhasusi (maalum) ambapo tokeo hilo ndilo lililopelekea kuteremshwa kwa aya hiyo, ama neno ÊÇÁæíá)) linafahamika kwa maana pana zaidi,yaani ðWanazuoni huifasiri aya na kuipa maana yenye mnasaba nao kinyume na ile maana dhahiri inavyoonekana.

Kuna baadhi ya watu wametabiri istilaha mbili hizo kama ifuatavyo:-

(ÊäÒíá  ( yaani ni dhahiri (ki-nje) na (ÊÇæíá ) yaani batini (kiundani), kwa sababu kama tukitizama aya kidhahiri tutaifahamu namna ya uteremshwaji wa aya hiyo, na kama tukitizama aya kibatini au kiundani tutaifahamu aya hiyo kwa maana iliyo pana zaidi.

Fudhayl bin Yasar akielezea kuhusu hadithi maarufu iliyonukuliwa kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w), hadithi hiyo ni hii ifuatayo:-

ãÇÝí ÇáÞÑÇä ÇíÉ ÇáÇ æ áåÇ ÙåÑ æÈØä   maana ya hadithi hiyo ni kama ifuatavyo:-

“katika Qur-ani hakuna aya isipokuwa ina maana yake ya kidhahiri na kibatini”.

Fudhayl bin Yasar alimuuliza Imam Sadiq (a.s) kuhusu hadithi hiyo. Imam alijibu kwa kusema:-

“Dhahiri ina maana na inaelezea namna ya uteremshwaji wa aya, na batini inaelezea aya hiyo kwa maana pana zaidi, katika matokeo yaliyotokea zama zilizopita au matokeo yatakayotokea zama zijazo”.

Imam anaendelea kwa kusema Qur-ani ni kitabu kilicho hai na kitakachobakia milele, kitabu hicho kitawaongoa na kuwafaidisha watu, na ni mfano wa jua na mwezi kila siku kitakuwa katika hali ya kuangaza. (rejea Basair Darajat, ukurasa wa 196, hadithi ya 7).

Na katika hadithi nyengine anasema:-

“Dhahiri ya aya inaelezea watu ambao aya ziliteremshwa kwa sababu yao wao, na batini za aya zinaelezea tabia za watu ambao zinafanana na tabia za watu ambao aya hizo ziliteremshwa kwa sababu yao wao. Ili kufafanua vizuri kipengele hicho sio vibaya kuelezea kwa kusema:-

Aya ambazo zimeteremshwa kutokana na sifa za mtu fulani haimaanishi ya kwamba aya hiyo inamhusu mtu huyo peke yake bali inawahusu watu wote. (rejea Tafsiri Ayash, juzuu ya 1, ukurasa wa 11, hadithi ya 4).

Kwa kuzingatia nadhari za Mafakihi kuhusiana na uteremshwaji wa aya za Qur-ani, au misingi ya uteremshwaji wa aya hizo, wamepata natija au hukumu ya kutowa fatuwa kuwa, kutokana na ufahamu wa aya,  na vipi unaweza kutumika ufahamu huo, basi ni lazima itazamwe aya hiyo katika maana kuu ya kijumla, na wala sio maana makhasusi (maalum) iliyopelekea uteremshwaji wa aya hiyo, (yaani pindi itakapokuwa aya ina maana kuu ya kijumla) lakini ikawa imeteremshwa kutokana na sababu malum (makhasusi), aya hiyo haitotumika peke yake kwa watu maalum (makhasusi) waliosababisha kuteremshwa kwa aya hiyo. kwa hiyo:-

Fakihi mwenye elimu ni lazima aweze kuweka kando baadhi ya vipengele maalum (makhasusi), na azingatie zaidi maana kuu ya aya hiyo na sio kuzingatia ya kwamba aya hiyo imeteremshwa kwa ajili ya mtu fulani, ijapokuwa kujua sababu za kuteremshwa aya kutamfanya mtu huyo afahamu zaidi maandiko au matini ya aya za Qur-ani. Ama kwa kuzingatia vipengele maalum tu haitopelekea kufahamu uteremshwaji wa Qur-ani. Kwa sababu hukumu za Mwenyeezi Mungu ni moja na zinawahusu watu wa zama zote, kwa hiyo kuzifasiri aya za Qur-ani kwa  maana kuu kumetabiriwa zaidi kuliko kuifasiri Qur-ani kwa kuzingatia vipengele maalum tu, (maneno hayo ni hukumu na fatuwa za Mafakihi).

NJIA ZA KUFAHAMU SABABU ZA UTEREMSHWAJI QUR-ANI

Kufahamu sababu za kuteremshwa Qur-ani ni jambo gumu sana kupita kiasi, kwa sababu Maulamaa wa zama zilizopita hawakudhibiti kitu chochote kinachuhusiana na uteremshwaji Qur-ani, pengine inawezekana sababu iliyowafanya Maulamaa hao wasidhibiti sababu ya uteremshwaji wa aya za Qur-ani ni kwamba kila kitu kilikuwa wazi na chenye kufahamika, kwa hiyo hawakuona umuhimu wa kutafuta sanadi zitakazoweza kuthibitisha hayo katika zama zijazo, lakini baadae kuliandikwa riwaya nyingi ambazo ni dhaifu na zisizokubalika kielimu, vile vile watu katika kipindi cha serikali ya bani Umayya waliandika riwaya nyingi ambazo sio zahihi na wakazinasibisha riwaya hizo kwa kuzifasiri na aya za Qur-ani vile ambavyo wanataka wenyewe.

Imenukuliwa na Imam Ahmad bin Hanbal ya kwamba kuna mambo matatu asili ambayo siyo sahihi, katika kuthibitishwa riwaya nayo ni :-

1.Riwaya ambazo zimeandikwa na zinaelezea kuhusu vita katika Uislamu.

2.Riwaya ambazo zinaelezea kuhusu fitna katika zama za mwisho.

3.Riwaya ambazo zinaelezea kuhusu kuifasiri Qur-ani.

Imam Badru Diyn Zarkeshiy amenukuu kutoka baadhi ya Wahakiki ya kwamba riwaya nyingi zinazohusiana na mambo hayo sio sahihi, lakini haimaanishi kuwa riwaya zote sio sahihi. (rejea Albur-han, juzuu ya 2, ukurasa wa 156). Sababu za kuteremshwa aya za Qur-ani zinafahamika kwa kunukuliwa riwaya, ama kwa bahati mbaya matokeo yaliyotokea katika zama zilizopita ambayo yanahusiana na uteremshwaji wa aya za Qur-ani hayakunukuliwa, hii imepelekea riwaya zilizonukuliwa na watu baada ya zama hizo zisikubalike kielimu kwani sio sahihi na zenye shaka ndani yake.

Bwana Wahidiy kuhusiana na sababu za uteremshwaji wa aya za Qur-ani anasema:-

“Haijaruhusiwa mtu yoyote kutowa nadharia inayohusiana na uteremshwaji wa aya za Qur-ani isipokuwa awe na sanadi (ushahidi) ya riwaya iliyo sahihi na yenye kukubalika, na riwaya hiyo iwe imenukuliwa na mtu ambaye alishuhudia matokeo yaliyotokea katika zama hizo, au iwe imenukuliwa na Matabiina, na wala hatakiwi mtu huyo kutowa nadharia yake mwenyewe.

Imenukuliwa kutoka kwa Ibni Abass ya kwamba Mtume Muhammad (s.a.w) amesema:-

“Jiepusheni na jizuilieni kunukuu hadithi isipokuwa mtakapokuwa na elimu sahihi ya kufahamu kile ambacho mnakinukuu, kwa sababu mtu yeyote atakayesema uongo juu yangu mimi na Qur-ani ameandaliwa moto mkali siku ya kiama”.

Bwana Muhammad bin Sayriyn anasema:-

“Nilimuuliza Ubayda kuhusiana na kuifasiri Qur-ani, Ubayda alinijibu kwa kusema wametoweka wale watu ambao walikuwa wakielewa na kufahamu sababu za kuteremshwa Qur-ani”.

Bwana Wahidiy anasema:-

“katika zama hizi kuna watu wengi sana ambao wanasema uongo ili kufikia katika malengo yao, ili kujua na kufahamu uhakika wa Qur-ani ni lazima kuchukua hadhari katika kutoa nadhari ambazo hazina dalili zozote. (rejea Asbabu Nuzuwl, ukurasa wa 4)

Bwana Jalali Diyn Suyutiy kutokana na nguvu na uwezo aliokuwa nao katika kunukuu riwaya hakuweza kukusanya hadithi zilizokuwa sahihi zaidi ya 250. (rejea Al-i-tqan, juzuu ya 4, ukurasa wa 214 na 257).

Lakini ni neema ilioje kumenukuliwa na kukusanywa riwaya nyingi zisizopungua 4000 ambazo ni sahihi kutoka kwa Ahlul-bayt (a.s). (riwaya hii imeelezewa na bwana Burhan, na kuna juzuu 10 hadi sasa ambazo tayari zimeshachapishwa).

Vitabu muhimu ambavyo tunaweza kuvitumia ambavyo vina uhakika na visivyo shaka ndani yake ili kufahamu sababu za kuteremshwa aya za Qur-ani ni hivi vifuatavyo:-

Jaamiul-bayan.Tabariy.

Addarul-Manthuwr. Suyutiy.

Maj-maul-bayan. Tabrasiy.

Atibyan. Sheikh Tuwsiy

Asbabu Nuzuwl. Wahiydiy.

Lababu Nuquwl. Suywtit.

Ama ni lazima tuwe makini katika kuvitalii vitabu hivyo, ili kuweza kupambanua maelezo ya riwaya zilizo sahihi na zile zilizokuwa sio sahihi kwa kutumia njia hizi:-

1.Sanadi ya riwaya ni lazima iwe imemalizikia na mtu ambaye ni mwenye uhakika na kukubaliwa katika dini, kwa mfano, awe ni katika watu wa Ahlulbayt (Maimamu), au awe ni katika Masahaba wema na waaminifu, mfano wa masahaba hao:-

Abdallah bin Masoud.

Ubayya bin Kaab.

Ibn Abbas.

Watu hao walikuwa ni mahiri sana katika masuala ya Qur-ani na ni wenye kukubaliwa na umati wote wa Mtume Muhammad (s.a.w). Au vile vile tunaweza kuwakubali watu waliokuwa wema na waaminifu baada ya kutoweka Mtume, mfano wa watu hao ni:-

Mujahid Said bin Jubeyr.

Said bin Musyyab.

Watu hao walikuwa ni wa kweli na waaminifu, na walikuwa hawasemi uongo katika kunukuu riwaya.

2. Riwaya zilizonukuliwa ni lazima ziwe zinafuatana na kukubaliana kimaudhui, yaani ijapokuwa riwaya zitakuwa zimenukuliwa kwa maneno tofauti lakini ni lazima ziwe zinaleta maana moja, hii itapelekea kuwa na uhakika na kukubalika kuwa riwaya hiyo ni sahihi.

3. Riwaya zilizonukuliwa ambazo zinaelezea sababu za kuteremshwa Qur-ani ni lazima ziwe hazina matatizo na ziwaondolee watu shaka, hii itapelekea kukubalika ukweli wa hadithi hiyo, hata kama itakuwa sanadi ya riwaya sio sahihi. (kutokana na istilaha za elimu ya hadithi).

WAANDISHI WA WAHYI

Imedaiwa ya kwamba Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa hajui kusoma wala kuandika, na katika kaumu yake hakuwa akijulikana kama mtu aliyesoma, na kwa sababu watu hawakumuona kuandika au kusoma walimwita .Çãí  Na Qur-ani kariym pia imemuelezea Nabii Muhammad (s.a.w) kwa kumnasibisha na neno hilo la Ummi. Allah (s.w) katika Qur-ani tukufu (Suratul-Al- Aaraf aya ya 157 na 158) anasema:-

ÇáøóÐöíäó íóÊøóÈöÚõæäó ÇáÑøóÓõæáó ÇáäøóÈöíøó ÇáÇõãøöíøó ÇáøóÐöì íóÌöÏõæäóåõ ãóßúÊõæÈÇð ÚöäÏóåõãú Ýöì ÇáÊøóæúÑóÇÉö æóÇáÅöäúÌöíáö íóÇúãõÑõåõã ÈöÇáúãóÚúÑõæÝö æóíóäúåóÇåõãú Úóäö ÇáúãõäßóÑö æóíõÍöáøõ áóåõãõ ÇáØøóíøöÈóÇÊö æóíõÍóÑøöãõ Úóáóíúåöãõ ÇáúÎóÈóÂÆöËó æóíóÖóÚõ Úóäúåõãú ÅöÕúÑóåõãú æóÇáÇóÛúáÇóáó ÇáøóÊöì ßóÇäóÊú Úóáóíúåöãú ÝóÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú Èöåö æóÚóÒøóÑõæåõ æóäóÕóÑõæåõ æóÇÊøóÈóÚõæÇú ÇáäøõæÑó ÇáøóÐöíó ÇõäÒöáó ãóÚóåõ ÇõæúáóÜÆößó åõãõ ÇáúãõÝúáöÍõæäó

 Þõáú íóÇ ÇóíøõåóÇ ÇáäøóÇÓõ Åöäøöì ÑóÓõæáõ ÇááåöÅöáóíúßõãú ÌóãöíÚÇð ÇáøóÐöì áóåõ ãõáúßõ ÇáÓøóãóÇæóÇÊö æóÇáÇóÑúÖö áÇ ÅöáóÜåó ÅöáÇøó åõæó íõÍúíöÜí æóíõãöíÊõ ÝóÂãöäõæÇú ÈöÇááåö æóÑóÓõæáöåö ÇáäøóÈöíøö ÇáÇõãøöíøö ÇáøóÐöì íõÄúãöäõ ÈöÇááåö æóßóáöãóÇÊöåö æóÇÊøóÈöÚõæåõ áóÚóáøóßõãú ÊóåúÊóÏõæäó

Maana ya aya hizo ni kama ifuatavyo:-

“Ambao wanamfuata Mtume, Nabii aliye Ummy (asiyejua kusoma wala kuandika, na juu ya hivi atafundisha mafundisho hayo ya ajabu ya Uislamu), ambao wanamuona ameandikwa kwao katika Tawrati na Injili ambaye anawaamrisha mema na anawakataza yaliyo mabaya, na kuwahalalishia vizuri na kuwaharamishia vibaya, na kuwaondolea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao (yaani sheria ngumu za zamani na mila za kikafiri). Basi wale waliomuamini yeye na kumuheshimu na kumsaidia na kuifuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye (yaani Qur-ani) hao ndio wenye kufaulu”.

“Sema (Ewe Nabii Muhammad): “Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyeezi Mungu kwenu nyinyi nyote; (Mwnyeezi Mungu) ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi, hapana aabudiwaye (kwa haki) ila yeye; yeye ndiye ahuishaye na ndiye afishaye.

Basi Muaminini Mwenyeezi Mungu na Mtume wake aliye Nabii Ummy, (asiyejua kusoma wala kuandika) ambaye humuamini Mwenyeezi Mungu na maneno yake. Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka”. Katika aya hiyo Neno Çãí limenasibishwa na linatokana na mjengeko wa neno Çã   likiwa na maana ya (mama) na neno hilo hutumika kwa mtu ambaye tangu siku aliyozaliwa na mama yake hakuwa na elimu (hakupata elimu).

Vile vile kuna maana nyengine iliyoelezewa kuhusu neno hilo (Ummy), na imenasibishwa na neno Çã ÇáÞÑí likiwa na maana ya mtaa wa mji wa Makka, na inaamaanisha mtu aliyezaliwa katika mji wa Makka”. Katika Qur-ani pia neno hilo limetumika katika mtindo tofauti kwa mfano, Allah (s.w) katika Qur-ani (Suratul-Jumua aya ya 2) anasema:-

åõæó ÇáøóÐöì ÈóÚóËó Ýöì ÇáÇõãøöíøöíäó ÑóÓõæáÇð ãøöäúåõãú íóÊúáõæ Úóáóíúåöãú ÂíóÇÊöåö æóíõÒóßøöíåöãú æóíõÚóáøöãõåõãõ ÇáúßöÊóÇÈó æóÇáúÍößúãóÉó æóÅöä ßóÇäõæÇ ãöä ÞóÈúáõ áóÝöì ÖóáÇóáò ãøõÈöíäò

Maana ya aya hiyo ni kama ifuatavyo:-

“Yeye ndiye aliyeleta Mtume katika watu wasiojua  kusoma, anayetokana na wao, awasomee Aya zake na kuwatakasa na kuwafunza kitabu na Hikima, (ilimu nyenginezo). Na kabla ya haya walikuwa katika upotofu (upotevu) ulio dhahiri”.

Inawezekana maana ya pili ya neno Ummy ikawa ni sahihi ama maana ya mwanzo ni mashuhuri na ni maarufu zaidi. Kwa sababu:-

1. Aya nyengine nyingi zinakubaliana na maana hiyo ya mwanzo. Allah (s.w) katika Qur-ani (Suratul-Albaqara aya ya 78) anasema:-

æóãöäúåõãú Çõãøöíøõæäó áÇó íóÚúáóãõæäó ÇáúßöÊóÇÈó ÅöáÇøó ÇóãóÇäöíøó æóÅöäú åõãú ÅöáÇøó íóÙõäøõæäó

“Maana ya aya hiyo ni kama ifuatavyo:-

Na wako miongoni mwao (hao Mayahudi) watu wasiojua kusoma; hawajui (kusoma na kufahamu) kitabu (cha Mwenyeezi Mungu; hawajui) isipokua tamaa tu za upuuzi nao hawana ila kudhani tu”.

Katika aya hii neno áÇó íóÚúáóãõæäó ÇáúßöÊóÇÈó kidhahiri limefasiriwa Çõãøöíøõæäó yaani (Ummy).

2. Kitu au tokeo lililoifanya Qur-ani kueleweka kuwa muujiza ni kutokusoma na kutokuandika na wala sio kutoweza kusoma na kuandika, kutokana na maelezo hayo basi itafahamika kwamba Mtume Muhammad (s.a.w) hakusoma wala kuandika, lakini hiyo sio sababu ya kuwa yeye hakuweza au hakujua kusoma wala kuandika.

Allah (s.w) katika Qur-ani (Suratul-Al-Ankabuut aya ya 48) anasema:-

ßõäÊó ÊóÊúáõæ ãöä ÞóÈúáöåö ãöä ßöÊóÇÈò æóáÇó ÊóÎõØøõåõ Èöíóãöíäößó ÅöÐÇð áÇøóÑúÊóÇÈó ÇáúãõÈúØöáõæäó

Maana ya aya hiyo ni kama ifuatavyo:-

“Na hakuwa mwenye kusoma kitabu chochote kabla ya hiki, wala hukukiandika kwa mkono wako wa kuume (kulia), ingekuwa hivyo wangefanya shaka wale wanaotaka kubadilisha (haki).

Aya hii inatoa dalili ya kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa hasomi wala kuandika lakini haimaanishi kuwa alikuwa hawezi kusoma na kuandika, na vile vile aya hiyo inatosheleza kuwathibitishia wale ambao wana madai ya kuwa Mtume hakuwa mwenye kujua kusoma wala kuandika, kwa hiyo hakuna njia tena ya watu hao kuendelea kuthibitisha madai yao hayo ambayo hayana dalili za kuyathibitishia.

Sheikh Tuwsiy katika kuifasiri aya hiyo anasema:-

Wafasiri wengi wamesema ya kwamba Mtume alikuwa hajui kuandika, lakini ukizingatia aya hiyo haileti maana hiyo, bali ina maana hii ya kwamba hakusoma wala kuandika, kwani kuna watu wengi hawaandiki lakini wana uwezo na wanaweza kuandika, na kidhahiri wanaonekana hawana elimu na hawajui kuandika, basi jambo linalofahamika katika aya hiyo ni kwamba Mtume hakusoma wala kuandika na alikuwa hana kawaida ya kuandika ijapokuwa alikuwa ana uwezo wa kufanya hivyo. (rejea Al-tibyan, juzuu ya 8, ukurasa wa 193).

Alame Tabatabai pia anaikubali nadharia hiyo (rejea Al-Miyzan, juzuu ya 16, ukurasa wa 145).

Kwa kuongezea:-

 kuwa na elimu ni jambo linalomfanya mtu awe amekamilika, na kutokuwa na elimu ni aibu, lakini Mtume Muhammad (s.a.w) amekamilika na kila kitu kutokana na neema au inaya ambayo amejaaliwa na kutunukiwa na Allah (s.w), kwa sababu yeye hakuwa mwenye kusoma kwa mwalimu yoyote katika maisha yake lakini alikuwa anajuwa kusoma na kuandika.

Basi ni jambo lisilowezekana nafsi ya Mtume kukosa sifa hizo.

Kutojidhihirisha kwa Mtume kuwa yeye ni mwenye elimu kulipelekea apate watu ambae watakuwa naye pamoja katika masuala ya uandishi wa Wahyi, sio katika mji wa Makka wala Madina kulikuwa kuna watu wengi ambao walikuwa na elimu, na Mtume aliwachagua watu hao katika kazi hiyo ya uandishi, mtu wa mwanzo aliyemchagua Mtume kuwa muandishi katika mji wa Makka ni Ali bin Abi-Talib naye aliendelea na kazi hiyo ya uandishi hadi siku ya mwisho ya uhai wa Mtume Muhammad (s.a.w).

Na Mtume alikuwa akimtanabahisha Imam Ali (a.s) aandike na kukithabiti kile ambacho kinateremshwa, ili kile ambacho kinateremshwa katika Qur-ani na  Wahyi kisiwe mbali na yeye.

Sulaym bi Qays Hilaliy anasema:-

“Nilikuwa katika msikiti wa mji wa Kufe pamoja na Imam Ali (a.s), na watu walikuwa wamemzunguka Imam Ali, Imam akasema:-

“Wakati huu ambapo mimi nipo miongoni mwenu ulizeni masuala kuhusiana na kitabu cha Mwenyeezi Mungu, naapa kwa Mola wangu hakuna aya yeyote aliyoteremshwa isipokuwa Mtume Muhammad (s.a.w) aliisoma akanisomesha mimi pamoja na kuifasiri kwa undani aya hiyo”.

Mmoja katika watu waliohudhuria katika msikiti huo alisimama na kumuuliza Imam Ali wakati ambapo ilipokuwa ikiteremshwa aya na wewe hukuwepo ulikuwa ukifanya nini? Imam Ali alimjibu kwa kusema:-

“pindi ambapo nilikuwa nikienda kuonana na Mtume Muhammad (s.a.w) Mtume alikuwa akisema:-

“Ewe Ali! Wakati ulipokuwa hupo kuliteremshwa aya, na Mtume hunisomesha aya hiyo kwa kuifasiri na kuichambua kwa undani kabisa. (rejea Saqife, ukurasa wa 213-214).

Mtu wa mwanzo aliyechaguliwa na Mtume kuwa muandishi wa Wahyi katika mji wa Madina ni bwana Ubayya bin Kaab Ansariy, bwana huyo alikuwa akijua kuandika tangu zama za ujahili, Ubayya bin Kaab ni mtu ambaye Mtume Muhammad (s.a.w) alimfundisha mtu huyo Qur-ani nzima, na katika kipindi ambacho Mtume alikuwa keshafariki mtu huyo alichaguliwa na Sayyidna Othmani kuwa kiongozi katika kuikusanya qur-ani ndani ya msahafu mmoja. Na wakati wowote pindi panapotokea matatizo nadhari ya bwana Ubayya ilikuwa ikiheshimiwa na ndiye aliyekuwa akitatuwa matatizo hayo. (rejea Tamhiyd, juzuu ya 1, ukurasa wa 340 -348).

Bwana Zeid bin Thabit alikuwa akiishi katika mji wa Madina na alikuwa ana nyumba karibu na anapoishi Mtume Muhammad (s.a.w), bwana huyo alikuwa akijua kuandika, na kila wakati ambapo Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa anahitajia mtu kwa ajili ya kumuandikia, pindi ambapo bwana Ubayya bin Kaab anapokuwa hayupo humwita bwana huyo Zeid bin Thabit ili kumuandikia, kidogo kidogo uandishi wa bwana huyo ukawa rasmi na Mtume Muhammad (s.a.w) alimtaka mtu huyo kuandika kwa lugha ya kiibria kwa sababu mtu huyo alikuwa akiielewa lugha hiyo (Kiibria ni lugha wanayotumia Mayahudi), na vile vile mtu huyo alikuwa akimsomea na Mtume barua ambazo zimeandikwa kwa lugha hiyo na baadae kuzijibu, kwa hiyo bwana Zaid bin Thabit alipata fursa hiyo ya uandishi kutokana na amri ya Mtume, na mara nyingi alikuwa ni msomaji wa barua ambazo zinatumwa.(rejea Masahaf Sajistani, ukurasa wa 3).

Kwa hiyo waandishi maarufu wa Wahyi ni

Imam Ali bin Abi Talib

Bwana Ubayya bin Kaab

Bwana Zeid bin Thabit

Mbali ya watu hao vile vile kuna watu wengine ambao walichukua nafasi ya pili katika uandishi.

Bwana Ibn athiyr anasema:-

“Mmoja katika watu muhimu na waliokuwa ni lazima wahudhurie katika uandishi ni Bwana Abdallah Bin Arqam Zuhriy, bwana huyo alikuwa na wadhifa wa kuandika barua, ama Imam Ali (a.s) yeye alikuwa ana wadhifa wa kuandika barua zinazohusiana na mambo ya ahadi na masuala ya suluhu.

Ibn Athiyr anaendelea kwa kusema:-

“Miongoni mwa watu ambao walikuwa ni waandishi maarufu wa Mtume Muhammad (s.a.w) ni:-

Makhalifa watatu kabla ya Imam Ali bin Abitaliba (karrama llahu waj-hahu).

Zeid bi Awam.

Khalid na Aban ambao ni watoto wa bwana Said bin Al-as.

Handhala bin Usayd

Aalai bin Hadharamiy

Khalid bin Walid

Abdallah bin Rawaahih

Muhammad bin Musalameh

Abdallah bin Abiy Suluwl

Mughayrat bin Shaab

Amruw bin Al-as

Muawiya bin Abusufiyan

Jaham au Jahiym bin Salat

Muayqab bin Abiy Fatima

Shar-habiyl bin Hasana

Hao ni katika watu ambao walikuwa na elimu zama hizo katika kabila la Kiarabu, na walikuwa wakijua kusoma na kuandika, na baadhi ya wakati ambapo kumetokea masuala muhimu Mtume Muhammad (s.a.w) huwatumia watu hao kwa ajili ya uandishi, ama waandishi walio rasmi na maarufu ni watu watatu ambao waliainishwa hapo mwanzo, na bwana Arqam na bwana Abdallah bin Zanjaniy wamewataja watu zaidi ya arobaini ambao walikuwa ni waandishi wa Wahyi. (rejea tarekhe Qur-ani, ukurasa wa 20-21). Ambapo watu hao walitakiwa kufanya kazi hiyo ya uandishi pindi ambapo kumetokea jambo au tokeo muhimu.

Njia zilizotumika katika uandishi ni kama hizi zifuatazo:-

Kila kitu ambacho kilipatikana na kinachoweza kutumiwa katika uandishi kilitumika. Kwa mfano:-

Waliandika katika vitu hivi vifuatavyo:-

1.Makozi ya mtende.

2.Iliandikwa katika mawe.

3.Kipande cha ngozi, majani au karatasi.

4.Ngozi iliyo tayari kwa ajili ya kuandikia.

Baada ya aya kumalizika kuandikwa huhifadhiwa katika nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w).

Baadhi ya Masahaba walikuwa wakipendelea kuwa nayo Qur-ani hiyo, hivyo walikuwa wakiandika katika vipande vya majani au vipande vya karatasi na kuihifadhi kwa ajili yao wenyewe, ama ilikuwa ni kawaida Qur-ani hiyo kuhifadhiwa katika kitambaa fulani na baadae hutundikwa katika ukuta. (rejea Tamhiyd, juzuu ya 1, ukurasa wa 288).

Aya za Qur-ani zilizokuwa zikiteremshwa zilihidhiwa kwa nidhamu na utaratibu mzuri, na kila sura iliteremshwa kwa kuanzia bismilahi rahmani rahiymi na ilitambulika kuwa sura hiyo imemalizika  wakati inaporemshwa sura nyengine (yaani kila sura ilianzia na bismilahi rahmani rahiymi na ilimalizika kwa kuanzia bismilahi rahmani rahiymi nyengine).

Na kwa kuanzia bismilahi rahmani rahiymi Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa akiwaeleza Masahaba zake kuwa sura ya mwanzo imeshamalizika, na kwa sababu hii basi kila sura ilihifadhiwa peke yake, na hakukuwa na utaratibu wowote, la umuhimu ni kwamba kila sura ilikuwa ikihifadhiwa peke yake.

SURA ZA MAKKA NA SURA ZA MADINA

Moja kati ya masuala muhimu ndani ya elimu ya Qur-ani ni kuzifahamu na kuzielewa sura za Makka na zile za Madina, sura za Makka ni zile sura ambazo aliteremshiwa Mtume alipokuwa Makka, na sura za Madina ni sura ambazo aliteremshiwa alipokuwa Madina.

Kuzipambanua sura za Makka na za Madina ni muhimu sana kutokana na dalili zifuatazo:-

A. Tunaweza kujua na kutambua elimu ya Tarehe pamoja na sheria za kiislamu kwa kuzipambanua aya za sura za Makka na zile za Madina.

B. Kuzifahamu aya zilizoteremshwa Makka na zile zilizoteremshwa Madina kuna umuhimu na faida kubwa  katika kutoa dalili za kifqhi zinazohusiana na mambo ya ahkamu, (hukumu za kiisalmu), kwa sababu kuna aya nyingi kama zitatizamwa kidhahiri zitaonekana zina hukumu za kisheria, lakini kwa kutokaka na kuwa aya hizo zimeteremshwa Makka, na wakati zilipokuwa zikiteremshwa masuala ya hukumu yalikuwa hayajainishwa na kutolewa hukumu, basi kutokana na sababu hizo hakuna budi Maulamaa na Mafaqihi wa kiislamu wazifafanue na kuzifasiri kwa undani aya kama hizo.

Kwa mfano:-

Masuala yanayozungumzia (taklif) wadhifa au wajibu unaowawajibikia Makafiri katika masuala ya hukumu za kisheria, masuala hayo yalileta mizozo na utatanishi mkubwa miongoni mwa Mafakikhi.

Baadhi ya Wanafaqihi wamewafikiana na wana nadharia ya kuwa, mpaka pale ambapo mtu aliye kafiri na akawa hajasilimu basi mtu huyo hana wadhifa wala wajibu wowote unaomuwajibikia kuutekeleza katika masuala ya hukumu za kisheria, na ili kuthibitisha nadharia zao wametumia dalili nyingi kwa kuthibitisha kauli yao hiyo katika riwaya mbali mbali.

Ama Wanafaqihi wengine wana nadharia hii:-

Ya kuwa watu ambao ni Makafiri hata akawa hajasilimu ana wadhifa na inamuwajibikia kuyatenda masuala ya hukumu ya kisheria, na wametoa dalili zao kwa kutumia aya ya Qur-ani ya (Suratul-Fussilat, Haa-mym Sajidah aya ya 7). Allah (s.w) katika sura hiyo anasema:-

ÇáøóÐöíäó áÇó íõÄúÊõæäó ÇáÒøóßóÇÉó æóåõã ÈöÇáÂÎöÑóÉö åõãú ßóÇÝöÑõæäó

Maana ya aya hiyo ni kama ifuatavyo:-

“Ambao hawatoi Zaka na wanaikanusha Akhera”.

Ufafanuzi wa aya hiyo ni kwamba makafiri sio wenye kutoa zaka na wanaikanusha akhera.

Mafaqihi waliokubaliana na nadharia hiyo wameghafilika kwa sababu Surat Fussilat ni katika sura za Makka, na faradhi au sheria za uwajibikaji wa kutoa zaka uliamriwa katika mji wa Madina.

Na kwa uthibitisho zaidi ni kwamba wakati ilipoteremshwa aya hiyo kulikuwa hakujatokewa hukumu na sheria za kutoa zaka hata kwa Waislamu, (waislamu walikuwa hawajafaradhiwa kutoa Zaka).

Kutokana na maelezo hayo basi itawezekana vipi makafiri wawajibikiwe na kutoa zaka?.

Na tuifafanue aya hiyo kwa undani kwa kuzingatia nukta mbili hizi:-

1. Kusudio lililokusudiwa hapo katika kutoa Zaka ni kutoa Sadaqa tu, ambapo washirikina haiwalazimikii kufanya hivyo, kwa sababu moja katika sharti za kutoa Sadaqa ni kutoa Sadaqa kwa ajili ya ridhaa ya Mwenyeezi Mungu, ukizingatia kwamba Washirikina au Makafiri hawana itikadi ya kumuamini Mwenyeezi Mungu.

2. Ama kuhusiana na kuwa Makafiri haiwalazimikii kutoa Zaka ni kutokana na kufru yao, na pindi iwapo watakuwa na imani na kusilimu basi inawawajibikia kutoa Zaka.(rejea Tafsiri Tabrasiy, juzuu ya 9, ukurasa wa 5). (rejea Al-Miyzan, juzuu ya 17, ukurasa wa 384).

C. Umuhimu mwengine wa kuweza kuzipambanua sura za Makka na za Madina ni kwa sababu tutaweza kutoa dalili zenye nguvu katika masuala ya elimu ya Kalamu, kuna aya nyingi zinazothibitisha kuwa na fadhila kwa watu wa Mtume (Ahlul-bayt). Ambazo nyingi zao zimeteremshwa Madina, kwa sababu mji wa Madina ndiko kulikokuwa na mijadala mingi. Baadhi ya watu vile vile wana nadharia ya kuwa sura na aya nyengine ambazo zinazungumzia kuhusu watu wa Mtume zimeteremshwa Makka, lakini hawana dalili zozote zinazoweza kuthibtisha nadharia zao hizo. Kutokana na maelezo hayo basi imefahamika kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuzifahamu sura za Makka na zile za Madina kwa sababu tutaweza kutoa dalili katika kuthibisha masuala ya Maimamu.

Kwa mfano natushuhudie aya hii ya (Suratul-Insan aya ya 7-12). Allah (s,w) anasema:-

Åöäøó ÇáÇóÈúÑóÇÑó íóÔúÑóÈõæäó ãöä ßóÇúÓò ßóÇäó ãöÒóÇÌõåóÇ ßóÇÝõæÑÇð

ÚóíúäÇð íóÔúÑóÈõ ÈöåóÇ ÚöÈóÇÏõ Çááåö íõÝóÌøöÑõæäóåóÇÊóÝúÌöíÑÇð

íõæÝõæäó ÈöÇáäøóÐúÑö æóíóÎóÇÝõæäó íóæúãÇð ßóÇäó ÔóÑøõåõãõÓúÊóØöíÑÇð

æóíõØúÚöãõæäó ÇáØøóÚóÇãó ÚóáÜٰí ÍõÈøöåö ãöÓúßöíäÇðæóíóÊöíãÇð æóÇóÓöíÑÇð

ÅöäøóãóÇ äõØúÚöãõßõãú áöæóÌúåö Çááåö áÇó äõÑöíÏõ ãöäßõãúÌóÒóÇÁ æóáÇó ÔõßõæÑÇð

ÅöäøóÇ äóÎóÇÝõ ãöä ÑøóÈøöäóÇ íóæúãÇð ÚóÈõæÓÇðÞóãúØóÑöíÑÇð

ÝóæóÞóÇåõãõ Çááåõ ÔóÑøó Ðٰáößó Çáúíóæúã æóáóÞøóÇåõãúäóÖúÑóÉð æóÓõÑõæÑÇð                                                                                                                                            æóÌóÒóÇåõã ÈöãóÇ ÕóÈóÑõæÇ ÌóäøóÉð æóÍóÑöíÑÇð

                                                                                                                           

Maana ya aya hizo ni kama ifuatavyo:-

“(Watu hao ni hawa) wanaotimiza wajibu (wao) na wanaiogopa siku ambayo shari yake itaenea (sana)”.

“Na huwalisha chakula masikini na mayatima na wafungwa, na hali ya kuwa wenyewe (wanakipenda chakula hicho)”.

“(Husema wenyewe katika nyoyo zao, wanawapa chakula hicho): Tunakulisheni kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyeezi Mungu (tu) hatutaki kwenu malipo wala shukurani.”

“hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu hiyo siku yenye shida na taabu.”

“Basi Mwenyeezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo na kuwakutanisha na neema na furaha.”

“Na atawajazi Mabustani (ya peponi) na maguo ya hariri, kwa sababu ya kusubiri (kwao).”

Maulamaa wamethibitisha kwamba chanzo na sababu za kuteremshwa sura hiyo ni kama hivi ifuatavyo:-

Imam Hussein (a.s) alishikwa na maradhi, (Imam Hussein (a.s) ni mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w) kwa binti yake Fatima binti Rasuli) Mtume Muhammad (s.a.w) pamoja na Masahaba wake walikwenda kumtizama na kumjulia hali mgonjwa huyo, Mtume baada ya kuona hali ya mgonjwa alimshauri na kumtaka Imam Ali (a.s) aweke nadhiri kwa allah (s.w) ili mwanawe apone na apate shafaa. Imam Ali alikubali ushauri huo na akaweka nadhiri ya kufunga siku tatu, siku ya mwanzo walipokuwa katika saumu (Bibi Fatima na Imam Ali) wakati walipokuwa wakitaka kuftari alitokea Masikini aliyekuwa akiomba msaada wa chakula, Imam Ali chakula ambacho walikuwa wamekitayarisha kwa ajili ya kuftari alimsaidia mtu huyo, siku ya pili vile vile wakiwa katika saumu wakati wanataka kuftari akatokea mtu yatima aliyekuwa akiomba msaada wa chakula, Imam vile vile alimpa mtu huyo chakula walichokitayarisha kwa ajili ya futari, siku ya tatu kama kawaida wakiwa tayari wanataka kuftari akatokea mfungwa aliyekuwa akitaka msaada wa chakula Imam Ali alimpa mtu huyo chakula na wao wakamaliza siku kwa kuftari mkate na maji. Alhamdulilah kwa uwezo wa Mwenyeezi Mungu Imam Hussein alipona na kupata shafaa.

Sheikh tabrasiy amethibitisha ya kuwa sura hii imeteremshwa Madina na ametowa dalili nyingi kutoka katika riwaya za Ahli Sunna, Ahli Shia, na vile vile amethibitisha kwa kutumia hadithi za watu wa Mtume (Ahlul-Bayt). Na dalili zote hizo zimekubaliwa na wafasiri pamoja na maulamaa wengi wa kidini. (rejea Tafsiri Tabrasiy, juzuu ya 10, ukurasa wa 404-406). (rejea Shawahid Tanziyl, ukurasa wa 229-315).

Bwana Abdallah bin Zubeir yeye amepinga nadharria za wafasiri na anasema kuwa sura hiyo ni ya Makka (rejea darul-Manthuwr, juzuu ya 6, ukurasa wa 297).

Lakini nadharia yake hiyo sio yenye kukubalika kwa sababu katika mji wa Makka kulikuwa hakuna wafungwa.

D. Matatizo mengi katika Qur-ani yanaweza kutatuliwa na kuthibitishwa kwa kueleweka sura za Makka na zile za Madina, kwa mfano katika  masuala ya äÓΠ . (Naskh ni kufutwa kwa hukumu za baadhi ya aya).

Kuna aya ambayo inasemekana imeteremshwa na kuelzea masuala ya ndoa ya (mut-a) au ndoa inayofungwa kwa muda mfupi, (aya hiyo iko katika Surat Nisaa aya ya 24), baadhi ya watu wana itikadi ya kuwa aya hiyo ni ãäÓæÎ  (yaani hukumu yake imefutwa) kwa kupitia - äÓÎ) ) - aya ya 5-7 iliyoko katika Surat- Almuuminun).

 Ili kufahamu masuala ya (Nasikh) na (Mansukh) ni vizuri kufafanua kwa ufupi kuhusiana na masuala hayo.

kuna baadhi ya aya zimeteremshwa na kutolewa hukumu, lakini baadae kukateremshwa aya nyengine ambazo zinafuta hukumu ya aya hizo ambazo zilitolewa hukumu mwanzo. Kwa mfano:-

Allah (s.w) katika (Suratul-Nisaa aya ya 24) anasema:-

æóÇáúãõÍúÕóäóÇÊõ ãöäó ÇáäøöÓóÇÁ ÅöáÇøó ãóÇ ãóáóßóÊú ÇóíúãóÇäõßõãú ßöÊóÇÈó Çááåö Úóáóíúßõãú æóÇõÍöáøó áóßõã ãøóÇ æóÑóÇÁ Ðٰáößõãú Çóä ÊóÈúÊóÛõæÇú ÈöÇóãúæóÇáößõã ãøõÍúÕöäöíäó ÛóíúÑó ãõÓóÇÝöÍöíäó ÝóãóÇ ÇÓúÊóãúÊóÚúÊõã Èöåö ãöäúåõäøó ÝóÂÊõæåõäøó ÇõÌõæÑóåõäøó ÝóÑöíÖóÉð æóáÇó ÌõäóÇÍó Úóáóíúßõãú ÝöíãóÇ ÊóÑóÇÖóíúÊõã Èöåö ãöä ÈóÚúÏö ÇáúÝóÑöíÖóÉö Åöäøó Çááøåó ßóÇäó ÚóáöíãÇð ÍóßöíãÇð

Maana ya aya hiyo ni kama ifuatavyo:-

“Na pia (mmeharamishiwa) wanawake wenye (waume zao) isipokuwa wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. (ndiyo) sharia ya Mwenyeezi Mungu juu yenu. Na mmehalalishiwa (kuoa wanawake) minghairi ya hawa. Muwatafute kwa mali zenu, kwa kuwaoa bila ya kufanya zina. Basi wale mnaowaowa miongoni mwao wapeni mahari yao yaliyolazimishwa. Wala si vibaya kwenu katika (kutoa) yale mliyoridhiana badala ya yale yaliyotajwa. Hakika Mwenyeezi Mungu ni Mjuzi na mwenye hikima.

Sababu ya kuteremshwa aya hiyo ni kuhusiana na ndoa ya (mut-a) au ndoa inayofungwa kwa muda fulani.

Aya nyengine ambayo imefuta hukumu ya aya hiyo ni (aya ya 5-7 ya Suratul-Al-Muuminun).

Allah (s.w) anasema:-

æóÇáøóÐöíäó åõãú áöÝõÑõæÌöåöãú ÍóÇÝöÙõæäó

ÅöáÇøó ÚóáÜٰí ÇóÒúæóÇÌöåöãú Çæú ãóÇ ãóáóßóÊú ÇóíúãóÇäõåõãú ÝóÅöäøóåõãú ÛóíúÑõ ãóáõæãöíäó

Ýóãóäö ÇÈúÊóÛóí æóÑóÇÁ Ðٰáößó ÝóÇõæúáóÆößó åõãõ ÇáúÚóÇÏõæäó

Maana ya aya hizo:-

“Na ambao tupu zao wanazilinda.”

“Isipokuwa kwa wake zao au kwa (wanawake) wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, (kulia). Basi hao ndio wasiolaumiwa.”

“(Lakini) anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka ya (Mwenyeezi Mungu).”

Nadhari hizo zilizotolewa hapo juu sio sahihi kutokana na dalili hizi zifuatazo:-

Moja: Aya ambayo wameielezea kuwa ni Nasikh iko katika Suratul-Al-Muuminun ni katika sura za Makka, na hakuna mtu yeyote aliyeifafanua aya hiyo kwa maelezo hayo.

Pili. Na aya ambayo wameitolea dalili ambayo iko katika Suratul-Nisaa ni katika sura ambazo ni za Madina, katika hali ambayo aya za (Nasikh) ni lazima zije baada ya aya za (Mansukh).